Habari mbaya inamhusu mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Averina
ambaye alikuwa akiombewa kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima la Nabii
Josephat Gwajima ambaye anadaiwa kufia nyumba ya kulala wageni (gesti)
ya My Fair iliyopo Kawe jijini Dar.
Tukio hilo lililoacha viulizo na kuzua minong’ono midomoni mwa wengi
lilijiri hivi karibuni ambapo mwanadada huyo aligundulika kuwa amefia
chumbani mishale ya saa 4:00 asubuhi.
Akizungumzia tukio hilo, mlinzi wa gesti hiyo aliyejitambulisha kwa
jina moja la Haruni alisema, mwanamke huyo alifikishwa mahali hapo
akionekana dhaifu kiafya, jambo lililosababisha kumuhoji mtu
aliyemfikisha hapo kuwa ni kipi kimemsibu.
“Huyu dada alipofikishwa hapa na mtu ninayemfahamu ambaye nasali naye
kanisa moja la Sabato, nikalazimika kumuhoji mama huyo aliyemleta ana
matatizo gani na kwa nini wamlaze gesti wakati ni mgonjwa, ndipo akanipa
mkasa mzima.
“Aliniambia huyu mama hana makazi maalum na alikuwa akisali kwa
Gwajima na kulala uwanjani hapo (Tanganyika Parkers, Kawe) huku hali
yake ikiwa si nzuri kiafya,” alisema mlinzi huyo.
Aliendelea kusema
kwamba hadi kufikia uamuzi wa kumlaza mahali hapo ni baada ya kuona hana
makazi huku akisaidiwa kupata matibabu.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa gesti hiyo, Apolinary Shayo alisema
siku ya tukio alipewa taarifa kuwa kuna mtu amefia ndani na alipojaribu
kumuhoji mtu aliyekuwa ameenda naye kwa kuwa alikuwepo mahali hapo kwa
lengo la kumpelekea chakula mgonjwa wake, akamueleza kuwa mama huyo
alikuwa akisumbuliwa na magonjwa tofauti (hayakutajwa) kwa muda mrefu.
Mwili wa mwanamke huyo ulichukuliwa na polisi wa Kituo cha Kawe, Dar
kwa uchunguzi zaidi na kutafuta ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi
ikidaiwa kwamba mama huyo alitokea mkoani (haikujulikana ni mkoa gani).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment