KOLETA AJAZA MATAMBARA KISA UJAUZITO, SOMA ZAIDI HAPA

Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema anapenda ujauzito kiasi cha kufikia hatua ya kujaza matambara tumboni ili awe na muonekano wa mjamzito.
Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
Akizungumza na paparazi wetu, Koleta alisema kwa jinsi anavyopenda ujauzito, akimuona mwanamke yeyote mjamzito anamfuata na kuzungumza naye hata kama hamfahamu na kama yuko jirani ataenda kukaa naye.
“Sijui kwa nini na kuna wakati mwingine naweka matambara  tumboni naweza kuzunguka nayo siku nzima kama mama mjamzito yaani huwa najicheka mwenyewe,” alisema Koleta huku akidai akitokea mwanaume watakayeendana basi atambebea ujauzito.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger