MOYO unahifadhi mengi! Msichana wa mjini
asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka
kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake
anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.
BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa
Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti
Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa
na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na
kumuomba afanye jitihada azae naye.
MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi
mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake
(Diamond).
“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na
Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa
anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa
mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu)
kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba
mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,”
alisema Anti Lulu.
Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani
amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na
Diamond.
IMANI
Anti Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali
japokuwa hawajawahi kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba
walishakutana na kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii...
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya
Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba
aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Niliambiwa alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni
zuri hivyo naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye
aliwahi kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.
BIFU?
Anti Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba
Wema atakasirika, hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha
naye bifu zito.
Alisema kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba
kikubwa anataka kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja
aendelee na maisha yake.
NENO!
“Najua Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa
sababu nimeamua na yeye ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani
hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito
aliyekuwa mpenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda
mfupi ilidaiwa kuchoropoka.Pia aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema
ambaye naye ilidaiwa ilichoropoka.
Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
SWALI LENYE HOJA!
Baadhi ya watu waliomsikia Anti Lulu akitangaza
ishu hiyo walijiuliza swali moja tu: ‘Hivi kweli Anti Lulu huyuhuyu
anaweza kuwa mama bora?’Diamond hakupatikana ili kufikishiwa ujumbe huo
na kujua namna alivyopokea taarifa hiyo ya Anti Lulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment