Mungu mkubwa! Baada ya kupitia kipindi kigumu cha
kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ kisha kunusuriwa, super lady kwenye
Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, hatimaye mambo yameanza
kumnyookea baada ya kulamba shavu tenda nono ya kulisha Hospitali ya
Mwananyamala, Dar.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa Wikienda, Ray C almaarufu
Kiuno Bila Mfupa amefungua bonge la ‘restauranti’ maeneo ya Mwananyamala
Hospital, ambapo amepata tenda ya kuwahudumia chakula wafanyakazi wa
hospitali hiyo na Idara ya Maji (Dawasa) ambapo anafanya kazi hiyo kwa
saa ishirini na nne na muda mwingi anakuwepo yeye mwenyewe.
“Bidada sasa hivi yupo njema sana. Kalamba shavu la kulisha Hospitali
ya Mwananyamala na Dawasa na hapo ni mchana na usiku so yupo bize
kinoma.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu waliusaka mgahawa
huo na kufanikiwa kuupata ambapo walimkuta Ray C akiwa bize kuhudumia
wateja ambapo alisema: “Namshukuru Mungu kwani nimepata tenda ya
kuwapikia chakula wafanyakazi wa Mwananyamala na wale wagonjwa ambao ni
waathirika wa madawa ya kulevya.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment