WIKI iliyopita tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alipokuwa
akimwelezea mchumba wake wa pili alivyokuwa hajatulia kiasi cha
kumchanganya na wanawake watatu tofauti. Leo anaelezea alivyokutana na
majanga mengine kwa mwanaume mwingine.
ENDELEA KUTOKA ILIPOISHIA…
“Huyu
mwanamke wa tatu baada ya kuondoka niliomba namba yake kwa mdogo wake
huyo mchumba, nikampigia na kumuomba nionane naye. Bila hiyana
alinikubalia, nilipoonana naye ndipo akanipasulia siri zote za yule
mwanaume, iliniuma sana.
“Kutokana na ubishi wangu, nikawa kama siaminiamini, akaniambia kama
siamini niende kuangalia albamu yake ambapo niliporudi kwao niliangalia
albamu yake na kukuta picha akiwa na wanawake tofauti tena kimahaba,
nilipotoka hapo sikurudi tena na aliponitafuta kwa simu nilimwambia
simuhitaji tena.
Mwandishi: Baada ya kuachana na huyo mchumba ulimpata mwingine?
“Ndiyo nilikutana na mwanaume anaitwa Kushi ambaye hatukuchunguzana muda
mrefu tukaoana, baada ya ndoa niligundua kwamba ni mlevi kupindukia,
siyo mwaminifu na alikuwa mkorofi sana hivyo wiki moja baada ya ndoa
tulipigana sana baa.
“Alikuwa akioa asubuhi na jioni kwani ndani ya ndoa yangu alioa
wanawake watano na kuwaacha, alikuwa ni tajiri sana lakini alipenda
starehe kupindukia hakuwa akinijali hata nguo ya ndani nilikosa nilikuwa
navaa zilizochanika, nakumbuka nikiwa na ujauzito aliniambia maisha ni
magumu niende nyumbani kwetu nirudi baada ya wiki mbili atakuwa
ameshapata hela ya kodi ya nyumba.
“Wiki mbili nilizomuacha alioa mwanamke mwingine ambaye waliachana
baada ya siku chache na kwenda Bagamoyo kwa mwanamke mwingine, maisha
yake yakawa ndiyo hayo.
“Siwezi
kumsahau huyu mwanaume na sitaki kumsikia kwa sababu aliniharibia dira
nzima ya maisha yangu kwani kwake ndipo nilianza kuvaa suruali, kwenda
klabu na baa wakati kabla ya hapo nilikuwa sivijui kabisa vitu hivi,
alikuwa hataki niwe na marafiki akiona nina rafiki wa kike anatembea
naye, kutokana na mateso hayo ilipofika mwaka 2001 tuliachana ikiwa ni
baada ya kuishi kwa mwaka mmoja tu katika ndoa.
Mwandishi: Je nini kiliendelea baada ya kuachana na Kushi?
“Nilianza maisha yangu mwenyewe mpaka mwaka 2003 nikakutana na
Msafiri Kondo (Solo Thang) ambaye tulikutana kwenye kazi baada ya
tamasha ndiyo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa muda mfupi nikapata
ujauzito ndipo akarudi Kushi na kuomba msamaha.
“Alipoona nakataa kumsamehe akachunguza niko na nani akagundua ndipo
alipomfuata Msafiri na kumtishia kwamba atamloga, nikamwambia Msafiri
asihofu lakini akawa bado ana wasiwasi lakini naye sikumchunguza sana
kabla kwani nilikuja kugundua kwamba alikuwa na mwanamke mwingine.
“Nilijifungua mtoto akiwa na siku tano Msafiri alisafiri na kwenda
Ulaya ambako huko alioa na kuzaa watoto wawili hivyo akawa ananitumia
matumizi ya mtoto mara mojamoja kwa hiyo kuanzia hapo nikawa nawalea
wanangu wawili mwenyewe.
“Nilikaa mwenyewe na wanangu kuanzia mwaka 2004-2006 ambapo mwaka
2006 nilirudi rasmi kwenye sanaa ya filamu kwani mwanzoni nilifanya
nikiwa shuleni.Wastara amezungumza vitu vingi kuhusu maisha yake.
Usikose sehemu ya mwisho ya makala haya wiki ijayo!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment