NAY WA MITEGO AKIRI KUZAA NA MSANII WA BONGO MUVI, PA AMWANIKA MTOTO WALIOZAA

Mambo hadharani! Baada ya kimya kirefu, staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mara ya kwanza amemwanika mtoto aliyezaa na msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na kukiri kwamba ni wa kwake.
Mtoto wa staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nay alisema kuwa anampenda mwanaye huyo na kwa sasa anaishi naye nyumbani kwake. Kimara-Baruti, Dar na ana umri wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Mama mzazi wa Munie ambaye ni msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ akipozi.
“Nampenda sana mwanangu ndiyo maana nimeamua kumchukua kwa mama yake Skaina na kuja kumlea kwangu, analelewa vizuri sana na mama yake ambaye ni Siwema namshukuru Mungu mwanangu anaendelea kukua, nafurahia sana kukaa na mwanangu karibu tofauti na alivyokuwa kwa mama yake,” alisema Nay wa Mitego.
‘Nay wa Mitego’ akiwa na mwanaye.
Skaina aliwahi kukiri kuwa mwananye huyo baba yake ni Nay lakini baada ya Nay kuulizwa alichengachenga hivyo sasa ameamua kumuweka wazi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger