Showing posts with label JOKATE. Show all posts
Showing posts with label JOKATE. Show all posts

HU NDIO UJIO MPYA WA JOKATE, NI SHIDAA

Kama unakumbuka mara ya kwanza kumuona Jokate anaimba basi wengi watasema walimwona kwenye video ya Kaka Dada aliyoimba na Lucci  wakati video yake ya kwanza ikiwa ni ile ya African Queen aliyoimba na AY. Hivi karibuni mrembo Jokate Mwengelo alienda nchini Kenya kwa ajili ya kufanya video ya single yake ya kwanza katika tasnia hii ya muziki. Video hii amefanya na mtangazaji mkenya, Nick  Mutuma ambapo aliimba nyimbo ya video hii kwa mara ya kwanza kwenye Serengeti Fiesta Mwanza .Hivi ni baadhi za vipande vya video hii mpya…
Jokate-mwengelo-na-nick-mutuma-vibe

Jokate-mwengelo-na-nick-mutuma-vibe-2
Jokate-mwengelo-na-nick-mutuma-2
Read more >>

LAANA: JOKATE ATUPIA PICHA MITANDAONI AKILIWA URODA, KWELI SASA AMEFULIA IONE HAPA MWENYEWE

huu mbinuko wa jokate ni shidaah bhana ndo maana midume kila siku macho juu kah

SOMA NA HII
Shilole aelezea jinsi anavyokunwa na Serengeti boyz wake, kumbe Mziwanda anampa mambo makubwa Shilole hebu yajue hapa===>>http://mdadisitz.blogspot.com/2014/09/shilole-mpenzi-wangu-ambaye-ni.html
Read more >>

JOKATE AFUNGUKA KUHUSU KUINGIA KWENYE BONGO FLEVA

 Jokate Mwengelo juzikati aliamua kujizamisha rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kupanda kwa mara ya kwanza katika Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, akiwa na madensa wake.
Mwanamitindo maarufu ambaye aliwika na lebo ya Kidoti, Jokate Mwengelo.
Ishu hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Agosti 10 mwaka huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo Jokate ‘aliwa-suprise’ mashabiki akiwa anajiamini akiimba na kutawala steji.Kwa muda wote akiwa jukwaani, mwanamitindo huyo alicheza staili sambamba na wanenguaji wake pasipo kupotea hata mara moja kama vile alianza zamani kuimba.
“Nina kipaji cha kuimba, na ndiyo maana nimekuwa nikiimba kanisani siku zote, muziki naupenda sema mwanzo nilishindwa kwenda na mambo mawili kwa wakati mmoja, ila sasa ndiyo nimezindua rasmi harakati za muziki na siku chache zijazo nitaachia video ya wimbo wangu nilioimba leo,” alisema Jokate
Read more >>

JOKATE NA DIAMOND WAONEANA AIBU!

Kwa mara ya kwanza tangu walipomwagana, mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wanadaiwa kuoneana aibu walipokutana laivu.
Mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pichani.
Akiwa na mtangazaji mwenzake, Edzen Jumanne, wikiendi iliyopita Jokate alidaiwa kushindwa kumbana Diamond kwa maswali wakati akimhoji kwenye kipindi kitakachoruka hewani hivi karibuni kupitia TV1.
Jokate  na ‘Diamond Platnumz’ wakipata ukodaki pamoja.
Baadaye Diamond alitupia mtandaoni picha akiwa na zilipendwa wake huyo hivyo kuibua mjadala mzito kuwa huenda bado wanapendana huku wenyewe wakipiga kimya.
Read more >>

KWELI JOKATE ANAPENDA KUIGA MASTAA WA MAMTONI?!!! ANGALIA PICHA HIZI

Read more >>

WAANGALIE WEMA NA JOKATE WALIPOKUTANA KWENYE NDEGE

Jokate aliwahi kukiri kwenye exclusive na millardayo.com kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond kwa muda usiozidi miezi miwili ambapo wakati yuko na Diamond zilitoka stori nyingi pia kuhusu uhusiano wa Wema na Jokate kuingia matatizoni.
Ni stori ambazo ziliandikwa sana na inawezekana mpaka leo watu wengine walikua wanaamini Jokate na Wema hawawezi kukaa meza moja ila Aug 9 2014 Wema Sepetu baada ya kuwasili Mwanza kwa ajili ya show ya Serengeti Fiesta 2014 baadae CCM Kirumba amepost hii picha.
Screen Shot 2014-08-09 at 2.25.00 PM 
Wakiwa kwenye ndege ya Fastjet Wema na Jokate wakitokea Dar es salaam walipiga selfie ambayo Wema ameipost kwenye instagram page yake na kuandika hayo maneno hapo chini akimaanisha wako poa sasa hivi.
Screen Shot 2014-08-09 at 2.25.16 PM
Read more >>

MPENZI MPYA WA JOKATE MWEGELO BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND.

Kupitia Mtandao wa Kijamii mrembo Jokate amemweka wazi mpenzi wake mpya na kuonyesha ni jinsi gani alivyo na furaha. This Is Love jamani Tuwaache wafanye yao... Beautiful Jokate In Love Again
Read more >>

MCHUMBA MPYA WA JOKATE MWAGELO HUYU HAPA, MUONE HAPA

Anajulikana kwa jina la Nick Mutuma ambaye ni msanii asiyeishiwa na vituko kutoka kenya ambaye inasemekana kuwa anadate na Msanii Jokate Mwagelo Kutoka Tanzania baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani ajulikanye kwa jina la Bridgette ,kupitia Instagram Nick alipost picha hiyo akiwa na Jokate huku wakionyesha kuwa na furaha kuwa pamoja
Read more >>

BAADA YA KUTANGAZA SIFA ZA MWANAUME AMPENDAE, NJEMBA KIBAO ZAGOMBEA KUMUOA JOKATE

Baada ya hivi karibuni mwanamitindo Jokate Mwegelo kutangaza kutafuta mchumba, idadi kubwa ya wanaume wamekuwa wakihaha kusaka mawasiliano naye huku kila mmoja akijinadi kivyake.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
Mara baada ya habari ya Jokate ya kutafuta mchumba kutoka kwenye gazeti hili wiki iliyopita, namba ya simu ya chumba chetu cha habari imekuwa bize kupokea simu za wanaume mbalimbali wakiomba kuunganishwa na mrembo huyo.
Hata hivyo, jitihada za kumuunganisha mmoja mmoja kwa mrembo huyo hazikufanyika ila kwa yoyote anayehisi ana vigezo na ana nia ya dhati ya kumuoa na si kumchezea afike katika ofisi zetu nasi tutamuelekeza njia sahihi ya kumpata.
Read more >>

BAADA YA KUCHEZA SANA, SASA JOKATE ASAKA MWANAUME WA KUMUOA, NA SI WAKUMCHEZEA

Katika kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku akitaja vigezo vya anayestahili kumuita mume.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema kuwa hana ‘mtu’ ila atakapotokea mwenye vigezo anavyotaka, hatakuwa na sababu ya kumkataa. “Kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, akitokea sina kipingamizi ila mbali na vigezo vingine awe na mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Jokate.
Jokate amekuwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu sana ila aliwahi kuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunder ya nchini Marekani.
Read more >>

JOKATE: AKU MIE, SIJAVUNJA NDOA YA DIDA

Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’ amefunguka kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’ kwani ni mshikaji wake na wanaheshimiana.
Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
'Dida' akiwa na Ezden.
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi hata siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni mshikaji wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”
Read more >>

HIZI NDIO PICHA ZA JOKATE AMBAZO ZINAMFANYA AONEKANE MZUR KULIKO WEMA SEPETU, ZICHEKI HAPA



The Best Photo Of All #TuzoZaWatu 

Read more >>

WAKUBWA TU: JOKATE AONYESHA SHANGA ZAKE NJENJE LIVE

Mwanamitindo maarufu na mbunifu wa mavazi nchini, Jokate mwegelo (pichani) akiwa kwenye pozi lenye utata..Watu na Viuno vyao Shanga pale kati
Comment Kiistaarabu Matusi na Kumchafua Mtu Hairuhusiwi

Read more >>

ALICHOPOSTI JOKATE KUHUSU CRISTIANO RONALDO, PIA AELEZA KWANINI ANAMKUBALI

ronaldo copyMichuano ya kombe la dunia imeendelea kuonyesha ukubwa wake kwa kuteka kila habari kuu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mabilioni ya watu duniani kote wakiwemo mastaa wakubwa wa kitaifa na kimataifa  wanafuatilia michuano hii ambayo ndio mikubwa kabisa katika soka duniani.
10402904_752093688187912_8259365943125327229_n-1
Mmoja wa mastaa wa kibongo ambaye ameonyesha kufuatilia michuano hii pamoja na wachezaji shiriki ni Jokate Mwegelo, ambaye mtangazaji wa TV, muigizaji na mmiliki wa lebo mavazi na fashion kiujumla ya Kidoti.
Tangu kuanza kwa michuano hiyo Jokate amekuwa akiposti posti tofauti kuhusiana na michuano hiyo, huku akionyesha namna anavyomkubali mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno inayoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri, anajituma uwanjani na anafunga magoli akiisadia timu anazochezea. Ana nidhamu ya kazi yake na akiifanya anaifanya kiuhakika na ndio maana tangu akiwa Manchester United nikajikuta namshabikia. Pamoja na hayo kitu kingine ambacho kinanifanya kumkubali Ronnie, ni namna ambavyo anajitoa kusaidia watu wasiojiweza, kama tulivyosikia juzi ametoa kiasi cha zaidi ya millioni 100 za kitanzania kusaidia matibabu ya mtoto aliyekuwa na matatizo fuvu la ubongo kujaa damu.”
10473394_249343711920920_4954243716833458720_nAkizungumzia michuano ya kombe la dunia, Kidoti alisema, “Kwenye michuano hii nilikuwa nasapoti timu za Afrika lakini zinaniangusha, hazichezi vizuri. Pia naisapoti Ureno kwa sababu ya nampenda Ronaldo, na Brazil pia nawapenda wanacheza vizuri hasa yule Neymar. Van Persie pia namkubali, lile goli alilofunga dhidi ya Spain kwa kichwa, aisee ni moja ya magoli bora kabisa.”
Read more >>

HAWA NDIO MASTAA WA KIBONGO AMBAO NI WATOTO WA KISHUA, WEMA NDANI YA NYUMBA

Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…
Celebrities-wa-bongo-wakishua-vibe-co-tz
Vanessa Mdee
Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.
Vanessa-Mdee-wakishua
Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.
Nisher-wakishua

Jokate Mwengelo
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.
Jokate-Mwengelo-wakishua

JANGA JINGINE KWA MBASHA: ALIZWA HATI ZA NYUMBA, VIWANJA

Lucci
Jina lake halisi anaitwa  Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini.  lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.
Lucci-wakishua

BINTI AOLEWA NA KIBABU KICHAWI , ALIYOYAKUTA NI MZITO, SOMA HAPA KUYAJUA

Wema Sepetu
Wema Sepetu ni msichana  anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma  elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University. 
Wema-Sepetu-wakishua

MZEE MAJUTO AFUNGUA, BAADA YA KUKAA KWA MUDA MREFU, SOMA ALICHOKISEMA HAPA

Read more >>

WAFAHAMU BIFU LA WEMA NA JOKATE LILIPOFIKIA, BASI UKWELI WOTE HUU HAPA

Kama mnavyojua tena mashosti hawa hapo awali walikuwa katika BIFU la kuchukuliana bwana ambae ni Diamond....Hii ilitokea baada ya Wema kumshutumu Jokate kutembea na mpenzi wake Diamond (Kabla Wema hajapigwa chini na Diamond)..
Katika hali isiyotegemewa wawili hawa kumbe hawana tena kinyongo..na wapo SAWA.....Hehehhee...Hii imejidihilisha wazi hapo jana baaba ya Wema Ku-comment kwenye picha ya Jokate huko INSTAGRAM...Soma comment hiyo hapo juu..then utajuani nini hasa namaanisha..
Read more >>

KIDOTI AIBUKA NA UBUNIFU MPYA

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ameibuka na ubunifu mpya wa sabuni ya kuogea inayokwenda kwa jina la Mo hiyo ikiwa ni baada ya kutesa na bidhaa ya ndala.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Jokate alisema uzinduzi wa sabuni hiyo unatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Juni 18, mwaka huu ambapo yeye na timu yake watatembea kwa miguu kutokea mjini (Posta) kuelekea Mbagala huku wakigawa zawadi kwa akina mama.
“Nashukuru nimeweza kubuni tena bidhaa nyingine, nataka kuwaambia wasichana wenzangu, wasilale. Tukitaka tunaweza kufanya makubwa. Nawashauri wapenzi wangu wakae barabarani kunisubiria nitapita na kundi langu la Kidoti ili niwapatie zawadi,” alisema Jokate.
Jokate Mwegelo.
Jokate amekuwa akibuni mitindo mbalimbali kama nguo, nywele na ndala lakini pia ni mwigizaji wa sinema za Kibongo.
Read more >>

JOKATE: ANASIFIKA KWA KUTOSUMBUA WAKATI AKIWA LOCATION KUPIGA PICHA ZA UMODO

hakika jokate ni modo wa ukweli africa na east africa kwa ujumla hivi karibuni tumefanikiwa kupata picha zake kali ambazo amewahi kupiga katika majalida mbali mbali, pia madirecta wamekuwa wakimsifia kwamba katika modo tz ambao hawasumbui katika swala zima la kuweka pozi anazoelekezwa na kamera man
 
Read more >>

NANI ZAIDI: WEMA SEPETU VS JOKATE MWENGELO

Wema Sepetu na jokate mwengelo ni kati ya wasichana warembo hapa bongo na role models. Wote mwanzo wao ulitokana na mashindano ya miss Tanzania ya mwaka 2006 ambapo wema sepetu aliibuka mshindi wa kwanza huku jokate akikamata namba mbili. Wema_na_Jokate 
 Najua huwezi kumuongelea wema sepetu au jokate bila kumuingiza diamond platnumz kidogo. Mnamo mwaka 2010 hadi 2011 diamond alianza kwanza kumdate mshindi wa kwanza wa miss tz jokate na kuachana nae na kuamia kwa mshindi wa pili yaani wema. Je, diamond nae alikua anataka kujibu swali tunaloliuliza ?  na kama amelijibu inabidi kushare jibu ilo na mashabiki tukajue.
wema-jokate-dating-diamond-www-vibe-co-tz-website Wema na jokate wote wanafanya movie na vigumu kujua nani zaidi katika uigizaji wa movie sababu kila mtu anasababu yake ya kumkubali mmoja wao.Twende kwenye fashion wema na jokate wamekua role models wa warembo wengi katika swala la uvaaji. wema-jokate-fashion-www-vibe-co-tz-website Tukija kwenye Ujasiriamali  wema na jokate hawapo nyuma. Wema alianzisha kampuni yake ya Endless Fame Films ambayo inatengeneza bongo movies. Pia wema anakipindi chake cha TV kinachoitwa In My Own Shoes kinachooneshwa na Channel 5 EATV. Tukija kwa Jokate mwengelo kikubwa kwake ni product ya Kidoti inayompa chati sana ukiachana na kazi ya utangazaji anayofanya kwenye channelO ya Afrika Kusini. wema-jokate-products-www-vibe-co-tz-copyrighted   Hata vibe magazine tuliliona hilo na kuamua kuwaweka wema na jokate katika cover page wakati ndio kwanza kuna issue tatu tu huku nyingine ikiwa ni kijana aliyewahi kuwadate wote diamond platnumz.
Read more >>

SIFA ZA MUME MTARAJIWA WA JOKATE NI HIZI HAPA, ZISOME KAMA WATAKA KUWA NI WEWE

MTOTO mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.
Mtoto mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo.
Akipia stori na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zote, awe anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alisema Jokate.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger