Showing posts with label RAY. Show all posts
Showing posts with label RAY. Show all posts

MAMA KANUMBA AFICHUA MAZITO YA RAY, MWANAYE, HAYA HAPA

BAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:
“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla  hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.”
Read more >>

RAY, JB WAMPIGIA SALUTI KAJALA, KISA KIZIMA HIKI HAPA

Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti muigizaji mwenzao,  Kajala Masanja kutokana na filamu fupi aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na waandishi wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa  Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.
Kajala Masanja akiwa na mwanaye, Paula.
“Kitu ambacho nimekipenda ni kwamba filamu ni fupi lakini ujumbe umeeleweka pia amefikiri kitu cha tofauti kabisa kwani hata watoto wa rika zote wanaweza kuangalia kwa ajili ya kujifunza,” alisema JB huku Ray akiunga mkono hoja.
Read more >>

RAY AFUNGUKA NA KUSEMA, "'SI LAZIMA KUJUA KINGEREZA KWANI MIE MUINGEREZA, HATA MESSI HAJUI'"




Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na watu mahir.
Read more >>

JOHARI AZIDI KUTESEKA PENZI LA RAY, AMWAMBIA IPO SIKU ATAMRUDIA TU, SOMA ALIYOFUNGUKA JOHARI HAPA

MKONGWE katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuendelea kuteseka na penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kunaswa akimzungumzia.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Viwanja vya Leaders Club kwenye uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo Johari alikuwa amekaa na kruu yake (huku  wakigonga ulabu) ndipo mmoja kati wenzake hao, akagusia stori za Ray kisha Johari alicheka na kusema ipo siku Ray atarejea katika mikono yake.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Ipo siku ambayo haijulikani tarehe wala mwaka Ray lazima atarudi katika mikono yangu kwani namfahamu sana Ray kuwa ni mtu wa kuruka lakini kwangu amefika,” alisikika Johari.
Read more >>

CHUCHU AMBAYE NI MPENZI WA RAY AZUA KIZAA ZAA BONGO MOVIE

  RAY ashindwa kumzika “Baba'ke” na JOHARI. Chuchu Hans 'atajwa'.
Read more >>

CHUCHU ARINGISHIA PENZI LA RAY, ONA MWENYEWE HAPA

STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans amedhihirisha kwamba ana mahaba niue kwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa kulinadi jina lake hadharani kwa kuvaa t-shirt iliyoandikwa; ‘Ray Kigosi’.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans akiringisha chata la msanii Mwenzake, 'Ray'.
Tukio hilo lilichukua nafasi wikiendi iliyopita kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar ambapo mwanadada huyo aliambatana na mashosti zake kushuhudia burudani tofauti ikiwemo mechi ya timu ya Bongo Fleva na Movies anayoichezea mpenzi wake.
Chuchu Hans akipozi.
Chuchu alivaa t-shirt ya njano ambayo mgongoni ilikuwa imeandikwa Ray Kigosi kitu ambacho hakuwahi kukifanya kabla.“Sioni tatizo kujinadi hadharani, atakayemaindi shauri yake, nafanya kitu roho inapenda bwana sijali maneno ya watu hata kidogo,” alifunguka Chuchu.usiku wa matumaini 2014..
Read more >>

UNDANI BIFU LA RAY, CHIKI, SOMA ZAIDI HAPA

BAADA ya kuibuka sintofahamu kati ya waigizaji wa Bongo Movies, Salum Mchoma ‘Chiki’ na Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki ameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’,
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Chiki alisema kuwa yeye na Ray hawakuwahi kuwa na bifu kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii isipokuwa walipishana kauli kidogo katika bethidei ya muigizaji Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar lakini waliyamaliza.
“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Salum Mchoma ‘Chiki’.
Kwenye bethidei hiyo, ilidaiwa kuwa Chiki aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alimpa maneno ya ‘madongo’ kumsisitiza atoe mkwanja ‘fedha’ nyingi kama zawadi kwa Dk. Cheni hali ambayo ilimuudhi Ray.
Imeandikwa na Maria Halimoja na Rhoda Josiah.
Read more >>

RAY ASHINDWA KUMZIKA BAM’DOGO WA JOHARI, KISA KIZIMA SOMA HAPA

MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.
Mkurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’
Mzee huyo alifariki katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya presha na figo yaliyokuwa yakimsumbua na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali wa filamu nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
 Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula akiwa msibani.
Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema:
“Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini,” alisema Ray.
Read more >>

MASHABIKI WALILIA PENZI LA RAY, JOHARI, HAWAMTAKI CHUCHU, SOMA HAPA

MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
Mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.
Read more >>

RAY NA CHUCHU HANS WACHAMBULIWA, SOMA KUJUA ZAIDI

 Account Maarufu ya Ukwelinauwazi kutoka Insta week hii imemlipua Ray na Kipenzi chake Chuchu Hans ..Jisomee Mwenyewe Hapo chini :
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger