MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’ amefungukia madai ya kumtenga msanii mwenzao, Coletha
Raymond ‘Koleta’ kipindi alipokuwa anaumwa.
Awali, madai yalipenyezwa kuwa, klabu hiyo ilimtenga Koleta kipindi
alipokuwa akiumwa ambapo alilazwa katika Hospitali ya Kairuki kwa
kilichodaiwa hakuwa na ushirikiano kati yake na wasanii wenzie.
Akikanusha taarifa hizo pamoja na kutomchangia fedha, Steve alisema:
“Tukianza kusema kila anayeumwa tuwe tunamchangia wanachama
watakimbia na mfuko tuliokuwa nao utaisha na tutashindwa kufikia
malengo, lakini sikupata taarifa za ugonjwa kuhusu Koleta na hata
ningezipata asingeachwa,” alisema Steve huku Koleta akisisitiza kuwa
anatengwa.
“Sijui kuna nini kinaendelea kwa upande wangu na sifahamu kwa nini
sipewi taarifa kwa wakati na uongozi wangu kama ilivyo kwa wasanii
wengine wa Bongo Movie, najisikia vibaya sana,” alisema Koleta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment