skip to main |
skip to sidebar
Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ ametoa kali ya
aina yake kwa kusema anapenda ujauzito kiasi cha kufikia hatua ya kujaza
matambara tumboni ili awe na muonekano wa mjamzito.
Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
Akizungumza na paparazi wetu, Koleta alisema kwa jinsi anavyopenda
ujauzito, akimuona mwanamke yeyote mjamzito anamfuata na kuzungumza naye
hata kama hamfahamu na kama yuko jirani ataenda kukaa naye.
“Sijui kwa nini na kuna wakati mwingine naweka matambara tumboni
naweza kuzunguka nayo siku nzima kama mama mjamzito yaani huwa najicheka
mwenyewe,” alisema Koleta huku akidai akitokea mwanaume watakayeendana
basi atambebea ujauzito.
Read more >>
MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’ amefungukia madai ya kumtenga msanii mwenzao, Coletha
Raymond ‘Koleta’ kipindi alipokuwa anaumwa.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ (mwenye suti).
Awali, madai yalipenyezwa kuwa, klabu hiyo ilimtenga Koleta kipindi
alipokuwa akiumwa ambapo alilazwa katika Hospitali ya Kairuki kwa
kilichodaiwa hakuwa na ushirikiano kati yake na wasanii wenzie.
Akikanusha taarifa hizo pamoja na kutomchangia fedha, Steve alisema:
Msanii wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
“Tukianza kusema kila anayeumwa tuwe tunamchangia wanachama
watakimbia na mfuko tuliokuwa nao utaisha na tutashindwa kufikia
malengo, lakini sikupata taarifa za ugonjwa kuhusu Koleta na hata
ningezipata asingeachwa,” alisema Steve huku Koleta akisisitiza kuwa
anatengwa.
“Sijui kuna nini kinaendelea kwa upande wangu na sifahamu kwa nini
sipewi taarifa kwa wakati na uongozi wangu kama ilivyo kwa wasanii
wengine wa Bongo Movie, najisikia vibaya sana,” alisema Koleta.
Read more >>
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’
amesema kwamba suala la yeye kuolewa siyo la leo wala kesho na kwamba
anakula ujana kwanza.
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Koleta alisema kwa sasa
hafikirii kabisa suala la kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa kuwa, kila
jambo na muda wake na bado Mungu hajamuonesha mwanawume wa kweli, ni
bora akaendelea kuwa ‘singo’.
“Kuolewa! Mmmh! Hapana kwanza, bado niponipo mpaka pale Mungu
atakaponipa mwanaume sahihi wa kuwa naye. Ndoa kujipanga bwana, si
kukurupuka tu, acha nile ujana kwanza,” alisema Koleta.
Read more >>