SPECIAL KWA WAPENDANAO



Marafiki kwa muda mrefu sana nimepotea, lakini nataka kuwahakikishia kwamba sasa nimerudi na mambo yataanza kuwa mazuri. Leo kwa kuanzia nataka niwape somo moja jepesi sana rafiki zangu, somo ambalo ni maalum kwa wapendao.

Nakupa sindano tatu muhimu za kuzingatia ili kumfanya mpenzi wako aendelee kukupenda.

1. Tabasamu lako ni taa na nuru ya kumvuta kwako. Hata kama amekasirika kiasi gani kwa kuachia tabasamu utamfanya akuone wewe kama sehemu yake maalumu ya kupata faraja.

2. Acha kumjibu kwa jazba, hata kama unajua kwamba yeye ndiye aliyekukosea.

3. Hakikisha kama mmekubaliana kula tunda, unampa hata una dharura kama 'simba' wanacheza au unaumwa. Achana na visingizio, kama kule kuna mvua, tumia mbinu nyingine kuhakikisha kwamba anafurahi na analala akiwa mwepesi ili siku inayofuata aweze kwenda kazini akiwa buheri wa afya.

Nisiwachoshe!

NAHISI KAMA NIMEANZA KWA KASI HIVI...Sasa washkaji, kama vipi kesho...bye...I love all.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger