Showing posts with label SKENDO. Show all posts
Showing posts with label SKENDO. Show all posts

FUMANIZI LA MWAKA: MKE AMBONDA HAWARA GESTI!


                           Hawara akipokea kichapo hevi kutoka kwa Mama la mama.

Kila kukicha kunaibuka vituko vingi duniani, wamo wanaosema huenda ni mwisho wa dunia! Mama mmoja almaarufu kwa jina la Mama la Mama anadaiwa kumbonda hawara wa mumewe baada ya kumwekea mtego wa fumanizi kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti).
Hawara akihaha ndani ya gesti ya White Paris (kimara) mara baada ya fumanizi.
SEKESEKE
Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.

ILIKUWAJE  WANAWAKE KWA WANAWAKE?
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.

Hawara  akidhibitiwa mara baada ya kunaswa katika mtego wa Mama la mama.
Ilidaiwa kuwa baada ya mumewe kuondoka na simu bila kujua haina laini, Mama la Mama aliiweka laini hiyo kwenye simu yake kisha akapitia namba kadhaa na kuitilia mashaka moja na alipopiga, akawa amepatia.Akamhadaa kwa kubadilisha sauti na kuzungumza kama mumewe.
MWANAMKE AINGIA MKENGE  
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni ‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.


Ilielezwa kwamba Mama la Mama alimdanganya hawara huyo kuwa endapo wataonana atapona hivyo akamwambia wakutane gesti hiyo kwa kuwa Mama la Mama ni mkazi wa Kimara, Dar.Ilisemekana kuwa Mama la Mama, huku akijifanya mwanaume alimuomba hawara huyo wakutane gesti kwani alikuwa amekumbuka penzi lake.
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka, akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.
Hawara akitoka gesti mara baada ya kuambulia fedheha kuu iliyomsibu.
NDANI YA CHUMBA CHA GESTI
Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa ndani na nje ya gesti.

KIPONDO
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Hawara kulia akiwa mapokezi ya gesti hiyo.
HAWARA AKODI CHUMBA KUKWEPA KIPIGO
Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala.

Akiwa kwenye mishemishe zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa kwani ni baamedi.
Umati wa watu ulioshuhudia laivu songombingo hilo.
MTUHUMIWA ANENA
Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani mwezi mmoja.

Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio Mama la Mama alikuwa ameondoka eneo hilo huku hawara akiendelea kutandika usingizi chumbani.
Read more >>

HAWA NDIO MAKAHABA WA JIJINI TANGA WANAOJIUZA KWA JERO JERO TU

BAADHI ya wakazi wa jijini Tanga, wameomba
uongozi wa Wilaya ya Tanga kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi, kuweka mkakati endelevu,
utakaodhibiti wimbi la vijana wa kike wanaojiuza
miili yao nyakati za usiku kwenye baadhi ya
barabara za katikati ya mji na bustani za
kupumzikia.Wamesema hatua hiyo, itasaidia
kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelezwa...
Read more >>

LUNDENGA NA MISS TANGA WAZICHAPA, SOMA ZAIDI HAPA

KW/RB/8441/2014 imemshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kwa madai ya kuzichapa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Miss Tanga 1997, Mona Faraja anayedaiwa kujeruhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga.
Ishu hiyo iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, nyumbani kwa Lundenga wakati wawili hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo, mara simu ya Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku, upi huo?
TUJINGE NA CHANZO
Mtoa habari wetu alisema kuwa, tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘kichenchede’ cha pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea.

Hashimu Lundenga akiwa katika kituo cha poisi cha Kawe.
“Mke wa Lundenga alikuwa na shauku ya kujua nani anayepiga simu ya mumewe muda huo na kwa nini mumewe haipokei lakini wakati akiendelea kujiuliza ndipo ikaingia meseji ambapo inadaiwa Lundenga alikwenda ‘fasta’ kwenye inbox na kuifutilia kwa mbali.
“Kitendo cha kufuta SMS hiyo nacho  kilitibua kabisa hali ya hewa, Mona akataka kujua kwa nini mumewe alikuwa hataki kupokea simu na SMS iliyoingia ilitoka wapi?
“Mona akawa mkali baada ya kuona haridhishwi na majibu ya mumewe ndipo alipoanza kutoa maneno yenye shutuma kwa mzee mzima ambapo naye uvumilivu ulimshinda kama binadamu wengine, wakaanza kutwangana,” kilisema chanzo hicho.

MKE AWAHI POLISI
Chanzo hakikuwa tayari kuweka ‘fullstop’, kiliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa, baada ya mke kuona anazidiwa kwa kushushiwa makonde mazito yaliyomvimbisha uso, usiku huohuo  alikimbilia Kituo cha Polisi Kawe, Dar kumripoti mumewe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga.
POLISI WAMKAMATA LUNDENGA
Mara baada ya mke kumaliza malalamiko yake kituoni hapo, saa chache baadaye polisi walifika nyumbani wakiwa na difenda ambapo walimchukua mlalamikiwa huyo hadi kituoni kujibu madai hayo.
“Polisi hawakuwa na maneno mengi, walipofika nyumbani walimkamata Lundenga na kwenda kumlaza kituoni kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria,” kilisema chanzo.

MAJIRANI WANENA
Baadhi ya majirani waliolitambua sakata hilo walionesha kushangazwa huku wakimhurumia Mona ambaye alikuwa ameumia usoni, hususan mzunguko wote wa jicho la kushoto.

MKE AINGIWA NA HURUMA
Wakati gazeti hili likiwa katika hatua za mwisho kuelekea mitamboni, Mona alidaiwa kuingiwa na huruma kwa kitendo cha kumlaza mumewe kituoni hivyo alikwenda kwa lengo la kumfutia mashitaka.

Hashimu Lundenga akiwa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja.
“Mke alimuonea huruma mumewe licha ya kupewa kipondo maana wamedumu kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa, si mchezo. Alikwenda Kawe kufuta kesi lakini polisi wakamkomalia kwamba ishu lazima ifike mahakamani,” kilisema chanzo.
Mwandishi wetu alifika kituoni hapo na kukuta polisi na Mona wakiendelea na mazungumzo lakini hadi tunakwenda mitamboni, Lundenga alikuwa bado anashikiliwa kituoni hapo.
MKE WA LUNDENGA
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu Mona kwa lengo la kutaka kumsikia anasemaje kuhusu madai hayo, lakini baada ya maelezo marefu ya mwandishi, alikata simu na baadaye kuizima kabisa!
Read more >>

FUMANIZI: KIGOGO SACCOS ANASWA GESTI AKIMLA URODA MTEJA WAKE AMBAE NI MKE WA MTU

KUNA madai kwamba, kigogo wa taasisi moja ya mikopo (Saccos) wilayani Bagamoyo, Pwani, Shabani Rajabu Mkali amenaswa gesti akiwa na mke wa mtu bila kujulikana waliingia kufanya nini, Amani linakupa picha nzima.
Kigogo wa taasisi moja ya mikopo (Saccos) wilayani Bagamoyo, Pwani, Shabani Rajabu Mkali  akiwa na mke wa mtu gesti.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara- Mwisho jijini Dar es Salaam ambapo mzee huyo alifika kwa nia ya dhati ya kukutana na mrembo huyo  aliyetambulika kwa jina la Rehema, anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule moja ya msingi mjini Bagamoyo.
Inadaiwa kuwa Rehema alikuwa akikutana na mzee huyo kwenye ofisi yake ya mikopo akitarajia kukopa fedha ili afanye biashara.
MTOA HABARI
Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers, mtoa habari wetu alisema mume wa mwanamke huyo, Matokeo Issa alikuwa na habari za mkewe kwenda kukutana na mzee huyo gesti, ndipo na yeye akafuatilia kwa nyuma ili kwenda kuwanasa.
“Wengine wanasema mume na mke walipanga kumnasa mzee huyo kwa vile alikuwa akimsumbua mara kwa mara, mke akamwambia mumewe.“Lakini wengine wanasema si kweli, mke alikwenda kwa kujificha lakini akaonekana na shemeji yake ambaye alimfuatilia kwa nyuma, alipoingia gesti akamwita kaka yake ndiyo wakamnasa,” kilisema chanzo hicho.
Kigogo Shabani Rajabu Mkali akiwa amesimama baada ya fumanizi.
Kikaendelea: “Lakini kwa taarifa zaidi mwoneni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Bakery, anaitwa Tatu Kitambulio, yeye anajua kila kitu maana baada ya mzee kunaswa aliitwa kuwa shahidi kwa vile ni mtu wa serikali.”
OFM YAMSAKA MJUMBE KITAMBULILO  
Ili kupata ukweli wa madai hayo, OFM walimtafuta Mjumbe Kitambulio ambaye alikuwa na haya ya kusema:“Ni kweli, ilikuwa Agosti 24, mwaka huu, nilifuatwa nyumbani na kuambiwa kule gesti kuna mzee amekutwa na mke wa mtu.
“Nilitoka hapa hadi gesti, nikakuta tukio lipo kweli. Mimi kama mjumbe ambaye nipo kwa niaba ya serikali, niliweka sawa mambo kwamba badala ya kufikishana mbali, wakubaliane. Aliyekutwa na mke wa mwenzake (mzee Mkali) akakubali kwamba atatoa shilingi milioni tatu ili mambo yaishe.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Bakery, Tatu Kitambulio akionesha picha ya kigogo akiwa na mke wa mtu .
“Ili kuweka ushahidi sawa alikubali kuweka ahadi yake kwenye maandishi. Aliandika anakubali kukutwa na mke wa Matokeo Issa na kwamba atalipa hizo pesa Agosti 26, mwaka huu kwa kumkabidhi mwenye mke.
“Basi, ilipofika Agosti 26, tukampigia simu kumuulizia, cha ajabu akasema kama mume anataka hizo pesa azifuate Bagamoyo lakini ajue kwamba analipwa na mke anabaki kwake yeye huyo mzee, tukashangaa sana.
“Tena mbaya zaidi aliacha maandishi yake kwangu kama mjumbe na mashahidi wawili, Waliondo Ali na Nasoro Abeid,” alisema mjumbe huyo.
OFM WAMSAKA MUME
Baada ya kuzungumza na mjumbe, OFM walimpata mume wa mwanamke huyo ambaye alisema:
“Nilikuwa nikimfuatilia mke wangu hatua kwa hatua baada ya kugundua kuwa ana nyendo zisizokubalika na yule mzee (Mkali). Kwanza mzee amekuwa akimwekea bili ya vitu mbalimbali mke wangu na kumpa fedha za matumizi kama kilainisho.
Waraka ukionesha Mkali 'akijikomiti' kwa maandishi kulipa faini kama fidia baada ya kunaswa.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Bakery, anaitwa Tatu KitambulioHata kama mke wangu alitaka mkopo iweje malipo yawe ngono?
“Kabla ya sakata hilo, nilianza kushangaa kuona mke wangu anakuwa bize tofauti na kipindi cha nyuma ndipo nikambana na akamtaja yule mzee.
“Za mwizi ni arobaini siku ikafika, mzee akampigia simu mke wangu ili wakutane  gesti huku akijua kufanya hivyo na mke wangu Rehema ni kosa kisheria.“Siku ya tukio mzee alitoka Bagamoyo anapoishi na kutimba Dar, akampigia simu, mimi nikajua na kumfuatilia mke wangu mpaka walipokuwa gesti na mimi nikaibuka na kuwanasa.”
INAVYODAIWA
Habari zinadai kuwa, mume alipowanasa wawili hao, mzee aliulizwa maswali yafuatayo:
Swali: Unafanya nini na huyu dada humu gesti?
Jibu: Nimekuja kumfundisha tuliyojifunza kwenye semina.
Swali: Unamfundisha kama nani yako?
Jibu: Nachukulia kama mwanangu nilikuja kumsaidia mizigo yake ili nitangulie nayo Bagamoyo.
Swali: Kwa nini unamwekea bili na kumpa fedha za matumizi?
Jibu: Mwanangu usinifanyie ukatili wowote mie nitalipa faini mtakayosema.
Swali: Utalipa shilingi ngapi kama faini?
Jibu: Semeni wenyewe.
Swali: Nataka utoe shilingi milioni tatu kama gharama nilizotumia kumsomesha mke wangu.
Jibu: Sawa, hakuna tatizo nitalipa baada ya siku tatu kuanzia leo mpaka kufikia tarehe 26, mwezi wa nane nitazileta kwa mjumbe.
MZEE MWENYEWE SASA
Baada ya kuzungumza na wote, OFM walimpigia simu mzee Mkali. Hali ikawa hivi:
OFM: Habari yako mzee? Shikamoo.
Mzee: Nani mwenzangu? Sema shida yako, nina mambo mengi.
OFM: Unamjua Rehema? Inadaiwa ulikutwa naye gesti pale Kimara Mwisho.
Mzee: Nasema uje mara moja huku Bagamoyo, vinginevyo nakuroga kijana.
Akakata simu.
Read more >>

DIAMOND ANUSURIKA KUPIGWA NA MASHABIKI HUKO UJERUMANI,POLISI WAMWOKOA,PROMOTA AINGIA MITINI, MKASA WOTE HUU HAPA

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
 Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diamond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba


Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 

Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"  link:

Read more >>

UDAKU: WASTARA JUMA AZICHAPA NA MUMEWE MAHAKAMANI

WIKI iliyopita katika makala haya tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alivyokimbizwa na mumewe wa kwanza na kuokolewa na difenda la polisi, TUENDELEE…



APEWA TALAKA

Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya purukushani hizo zote?
“Zilipita siku tatu mume wangu alinipigia simu akiwa na dada yake na kunitamkia kwamba ameniacha kwa talaka tatu na huyo dada yake ndiye shahidi na hiyo ilikuwa mwaka 1999.
“Haikupita miezi miwili alikuja nyumbani na kuandika talaka tatu za maandishi hivyo nikawa nipo tu nyumbani na wakati misukosuko yote ikiendelea, mama yangu alikuwa ameshafariki.

WASULUHISHWA
Mwandishi: Kwa hiyo katika kupewa talaka hizo hamkurudiana tena?
“Baada ya kunipa talaka kwenye simu wazazi wake walikuja kusuluhisha tukarudiana akaja kumchukua mtoto na akaenda kukaa naye Zanzibar huku mimi nikiwa nimepata kazi ambapo mwanangu alikaa huko kwa mwaka mmoja nilipoenda kumuona nikakuta ana utapia mlo ukweli nilisikia uchungu, niliwaambia namchukua mwanangu akanipokonya na kwenda kujifungia naye chumbani ambako nilienda na kuvunja mlango nikamchukua mtoto kwa nguvu ndipo alipokaa kwa miezi miwili akaja kuniandikia talaka ya maandishi.

APATA MCHUMBA MWINGINE
Mwandishi: Je baada ya kupewa talaka ulipata mchumba mwingine?

“Ndiyo nilipata mchumba ambaye kwa upande mwingine ni ndugu yetu ambaye alikuwa anaishi hukohuko Zanzibar lakini nilishangaa siku moja nikiwa naye pamoja na ndugu zangu wengine tumetoka kutembea, tulipofika nyumbani polisi wakaingia na kutuulizia mimi na yule mchumba ambapo walituchukua mpaka kituoni na nilipohoji walisema kwamba mume huyo wa zamani amenifuma na mwanaume mwingine wakati yeye ndiye mume wangu.


Wastara Juma akipozi.
“Tulikaa selo mpaka familia zote mbili zilipokuja na kuzungumza lakini hawakufikia muafaka, nikaomba ile kesi ipelekwe mahakamani kwa sababu sikuwa mke wa mtu, tukaenda mahakamani yule kijana ambaye ndiyo tulikuwa tunaanza uchumba yeye hakuwa na makosa tukabaki mimi na huyo mwanaume.

“Ilikuwa ni kama sinema kwani kila tulipokuwa tukikutana mahakamani tulikuwa tunapigana sana mpaka mahakama ikaamua kutuhamishia kwenye mahakama ya Kadhi (inayoshughulika na masuala ya ndoa) ambapo mwanaume huyo alidai kwamba anataka arudishiwe mahari yake nikaomba kesi ihamishiwe Dar, nikakubaliwa.

“Kabla sijafika Dar nikakuta ameshaniwahi na kwenda BAKWATA ambako alitakiwa anipe talaka lakini akaandika majina tu na kuondoka, Bakwata walinisaidia tukapeleka mahakamani ambapo tangazo la mahakama kutoa talaka lilitangazwa kwenye magazeti ya serikali kwa siku 39 ili mwenye pingamizi apeleke lakini hakuna aliyejitokeza hivyo nikapewa talaka na mahakama.

Mwandishi: Baada ya kumalizana na mumeo huyo uliendelea tena na yule mchumba?


“Niliendelea naye lakini tukiwa kwenye kuchunguzana siku moja nilikwenda kumtembelea kwao akaja mwanamke akawa anazungumza maneno mengi yakimhusu huyo mchumba kumbe alikuwa ni mwanamke wake, alipoondoka huyo jioni yake akaja mwingine akiwa anamuulizia na kesho yake akaja wa tatu ambaye alikuwa akilalamika kwamba huyo mwanaume anasikia ana mchumba wakati yeye ni mwanamke wake
Read more >>

RIHANNA NA BEYONCE NI WASAGAJI, SHUHUDIA MWENYEWE HAPA

Read more >>

LAANA: MWANAFUNZI WA CHUO AKIWA NA KANGA MOKO AKITOKA KUOGA BAFUNI

DENTI HUYU AMEAMUA KUTUONYESHA PICHA AKIWA AMEVAA KANGA TU ETI DAH ILA AWA KINA DADA WA CHUO AKILI ZIMEWARUKA KIUKWELI DAH
Read more >>

LAANA: WAKUTWA WAKIJIANDAA KULANA URODA HADHARANI, SOMA ZAIDI HAPA

Kweli dunia ina mambo, kapo hii wakiwa kwenye maandalizi
ya pasaka, walienda kwenye baa moja kupata moja baridi moja moto, ndipo mizuka ilipowapanda na kujikuta wakifanya uchafu wao bila kujali wanao wazunguka
Read more >>

MAKAHABA WANASWA WAKIWA WANAJIUZA MCHANA KWEUPEE, WAONE HAPA






Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata akinadada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu kama Machangudoa katika eneo la Sinza.

Picha hizi ( juu) zinaonesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria
Read more >>

LAANA: CHANGUDOA AWEKWA KITIMOTO BAADA YA KUFUMWA AKILIWA URODA

HILI kweli ni sekeseke la Idd el Fitr. Wakati changudoa mmoja akinaswa na kumwagiwa maji na wananchi waliochoshwa na vitendo vya ukahaba vinavyofanywa jirani na makazi yao, msichana mwingine aliokotwa akiwa amelewa chakari na kudhaniwa kuwa na mapepo, maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar Jumanne hii.
changudoa anaswa na njemba na kumwagiwa maji ya moto.
Katika tukio la kwanza lililotokea Idd Mosi, wakazi wa maeneo ya Afrikasana, waliamua kuweka mtego na kumnasa changudoa aliyekutwa na mteja wake wakimaliza haja zao uchochoroni, wakiwa wametandika boksi chini.
“Yaani tumechoshwa na hawa machangudoa, inafikia hatua tunashindwa kulala kwa sababu ya miguno yao ya kimapenzi, hata watoto wanashtuka usingizini kwa sababu ya mambo hayo, ni hatari kwani wanaweza kujifunza ufuska, tumeamua kuwanasa leo jamani na itakuwa fundisho kwao,” alilalamika mmoja wa majirani hao.
Huku timu ya Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ya Global Publishers ikiwa ‘beneti’ na majirani hao, ilishuhudia wawili hao wakikamatwa na kupewa adhabu ya kulowanishwa kwa maji ya moto ambapo nguo zao zililoa chapachapa.
Wakati changudoa huyo akipewa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa wenzake wanaokesha pembezoni mwa barabara ya Shekilango, msichana mwingine anayedhaniwa kuwa alilewa kupita kiasi, alikutwa akiwa amezungukwa na watu nje ya baa maarufu ya Corner.Changudoa huyo akijuta baada ya tukio hilo.
Kundi kubwa la watu lilimzunguka mwanamke huyo kutokana na vitendo vyake kuashiria alikuwa amelewa bwii, wengine wakiamini alikuwa na mapepo hivyo kutaka kujua namna ya kumsaidia.
“Huyu dada jamani itakuwa majini yake tu yanamsumbua, si unajua watu wengine majini yao hayapendezwi na ulevi uliozidi kiwango, maana mtu mwenyewe haeleweki, tukimshika kumsaidia anataka kuturukia sasa sijui tufanyaje,” alisikika kijana mmoja akisema.
Hata hivyo, baadhi ya vijana waliokuwa eneo hilo walionekana kupanga mbinu za kumchukuwa msichana huyo na kwenda kumfanyizia, kitu kilichoshtukiwa na mabaunsa wa baa hiyo ambao walimpandisha kwenye Bajaj na kumkimbiza Kituo cha Polisi Mabatini ambako baada ya askari kuwasikiliza, walishauri apelekwe hospitalini.Binti anusurika kubakwa baada ya kulewa chakali.
Alipelekwa Hospitali ya Palestina ambako baada ya kupimwa, alionekana kunywa pombe kali kupindukia, hivyo kuwekewa dripu.
Read more >>

LAANA: BINTI WA DARASA LA SABA AKURUPUSHWA GUEST KAMA ALIVYO, SOMA ZAIDI HAPA



Askari wa jeshi la polisi na wasamaria wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba moja ya shule ya msingi Manispaa ya Morogoro, binti huyo anadaiwa  kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi wakati akipelekwa kituo kidogo cha polisi. Kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na mapenzi na masomo.
Wasamalia wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba Manispaa ya Morogoro baada ya kumnusuru na kipigo kutoka kwa kundi la wananchi wenye hasira waliotaka kufuatia binti huyu kudaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi mkoani Morogoro.
Read more >>

AIBUU MSANII HUSUIN MACHOZI AFUMANIWA AKIZINI NA MKE WA MWANASIASA MKONGWE NCHINI KENYA



Hit maker wa  ‘Kwa Ajili Yako’, Hussein Machozi aliyekuwa ameweka kambi na kukubalika sana nchini Kenya anadaiwa kuwa amefumaniwa na mke wa mwanasiasa wa nchini humo na kupewa masaa 24 kuvuka mpaka wa Kenya.
Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Hussein Machozi alikuwa anatembea na mwanamke wa mwanasiasa huyo wa Mombasa kwa muda mrefu kwa siri huku wakiwa na mipango mikubwa ikiwa ni
pamoja na kununua nyumba.
Lakini mapenzi ni kikohozi, siri hiyo ilimfikia mwanasiasa huyo baada ya kushtukia pale alipoona ujumbe usio wa kawaida kwenye simu ya mkewe kwa njia ya WhatsApp.
Mwanasiasa huyo ambaye anadaiwa kuwa mtu anaesafiri mara kwa mara  kufanya biashara na kushughulikia mambo ya siasa aliamua kuweka mtego ambao ulimnasa mwizi wake na kumtia mikononi mwake.
Gazeti hilo linaeleza kuwa liliongea na rafiki wa karibu wa Hussein Machozi wa Mombasa anaefahamika kwa jina maarufu Notystee na alikiri kutokea kwa tukio hilo.

“Nilishtuka pale nilipopokea simu kutoka kwa Hussein Machozi akiniambia kuwa alikuwa katika tatizo. Aliniambia mapema kuwa anaenda kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake lakini sikujua kitu ambacho kingetokea.”
Hata hivyo, Hussein Machozi anaonekana bado yuko nchini Kenya kwa mujibu wa chanzo chetu.

Read more >>

LAANA: MAMA NA MWANAYE WAPIGANA KUGOMBEA MWANAUME....NI AIBU KUONA HAPA.

blacks-fighting
A 42-year- old housewife in Asaba, Delta State on Sunday, engaged her 17 year-old daughter in a fight for allegedly snatching her boyfriend.Eyewitness said that a scene was created around St. Brigid’s Girls College, Asaba, Sunday afternoon after both of them exchanged blows
Read more >>

FUMANIZI: NJEMBAA YAFUMANIWA AKIMLA URODA MKE WA MTU, ONA MWWENYEWE MKASA MZIMA NA BARUA YA MSAMAHA ALIYOIANDIKA

TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:

Kelvin (kulia)'akidili' kisawasawa na mjomba wake.
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin asizidi kumjeruhi mjomba wake.
OFM KAZINI, AIBU!
Kufuatia taarifa hiyo, mkuu wa zamu wa OFM aliwaagiza mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walitumia muda usiozidi robo saa kutoka walipokuwa kufika eneo la tukio ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!

Mjomba akiwa chumba cha gesti mara baada ya mkong'oto 'hevi' kutoka kwa mpwa wake.
PICHA ZA TUKIO
Mapaparazi wetu bila kuzubaa nao walianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.

MKE ATIMKA KINYEMELA
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.

...Mjomba taratiiibu 'akirejesha' mavazi mwilini mwake.
MLINZI WA GESTI
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.

MJOMBA MTU AGOMA KWENDA POLISI
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.

Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake.
CHONDECHONDE KELVIN
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.

MJOMBA ‘AJIKOMITI’ KIMAANDISHI
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.

Sehemu ya nyaraka ikionyesha mjomba 'akijikomiti' kimaandishi.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.
MGONI AGEUKA NA KWENDA KUFUNGUA KESI
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.

KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa sababu kisa hiki kinadaiwa kufikishwa polisi na Joseph, magazeti pendwa ya Global yataendelea kukifuatilia ili kujua mwisho wake. Endelea kusoma.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger