Showing posts with label KANUMBA. Show all posts
Showing posts with label KANUMBA. Show all posts

MAMA KANUMBA AFICHUA MAZITO YA RAY, MWANAYE, HAYA HAPA

BAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:
“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla  hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.”
Read more >>

BAADA YA KIMYA KIREFU, HATIMAYE KANUMBA THE GREAT YAKARABATIWA

BAADA ya kampuni ya marehemu Steven Kanumba, Kanumba The Great Film kudaiwa kufungwa, sasa imekarabatiwa na kuanza kazi upya.
Marehemu Steven Kanumba, Kanumba The Great enzi za uhai wake.
Mwanahabari wetu alifika kwenye ofisi hizo Jumatano iliyopita ambapo alishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walifanyia usafi vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuanza kazi upya.
“Tulifunga kwa muda lakini kwa sasa tumerudi kivingine baada ya kufanya maboresho katika ofisi, hivyo mashabiki wa Kanumba The Great Film wategemee makubwa,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao huku akiomba kustiriwa jina.
Read more >>

BABA KANUMBA: NAKUOMBA SASA MAMA KANUMBA UACHE NJAA

BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.
Baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba.
Akipiga stori na paparazi wetu, Baba Kanumba alisema anashangazwa na tabia ya mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini Shinyanga ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.
“Namshangaa mama Kanumba ni njaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha ukoo wa Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila sababu za msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akijibu tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote aende mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani mimi si mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba nilijiendea tu,” alisema.
Read more >>

VALENTINE YAMFANYA LULU KUKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA

WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.
Marehemu Steven Kanumba.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na haiwezekani tena,” alisema Lulu.
Hata hivyo, alipobanwa amtaje, staa huyo ambaye ni sura ya mauzo ya filamu za Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012, siku ambayo kamwe hawezi kuisahau maishani mwake.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger