Showing posts with label MAJUTO. Show all posts
Showing posts with label MAJUTO. Show all posts

MAJUTO AJIINGIZA KWENYE SISAS, SASA KUOMBEA UBUNGE 2015


Msanii wa vichekesho anayeongoza kwa kufanya filamu nyingi zinazowakuna mashabiki wengi sana kwa sasa majuto ametangaza rasmi lengo lake la kuwania ubunge 2015 jimbo moja wapo mkaoni Tanga akiongea alisema

”Nimewatumikia kwa muda sasa wapezi wangu na kuwapa kile wanachohitaji kwa kupitia sanaa yangu, umefikia wakati nataka nioneshe uwezo wangu wa kufanya kitu kingine na nipo kwenye harakati za kuwania Ubunge mwaka 2015 Jimbo mojawapo mkoani kwangu Tanga. Lakini kwa sasa siwezi kuongea sana wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi ila kwa sasa mashabiki wangu wajiandae kunipigia kura za kutosha.”
Read more >>

MZEE MAJUTO AZUNGUMZA MANENO YA KUSIKITISHA, NI KUWAALIKA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WAKE

NI Wikiendi nyingine ambayo mapaparazi wetu, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ Musa Mateja ‘Toz’ na Richard Bukos Mpigapicha Mkuu walijiachia viwanja mbalimbali kuwinda yaliyokuwa yakijiri na kumjuza moja kwa moja mkuu wao, Oscar Ndauka aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Msanii mkongwe na mkali wa maigizo na vichekesho, mzee Majuto (mwenye suti nyeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na mastaa wengine waliotunukiwa tuzo pia.
Akiwa ofisini Mkuu anaangalia saa na kubaini kuwa ni mida ya vijana wake kuwa viwanja hivyo anaamua kumtwangia Musa Mateja aliyekuwa Serena Hoteli ambapo kulikuwa na hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu.
Saa 2:52 usiku
Mateja: Haloo ... naam mkuu wangu, nakupata bila mikwaruzo.
Makao Makuu: Haya niambie ushafika Serena kwenye hiyo hafla?
Mateja: Mkuu wangu nimefika hapa muda si mrefu nilipitia nyumbani kwa Aunt Ezekiel kulikuwa na shughuli, Wema Sepetu na mastaa wengine wa kike walikuwa wakimtunza mwenzao beseni baada ya kujifungua salama.

Makao Makuu: Mambo yalikuwaje huko?
Mateja: Mkuu huko ilikuwa ni minyonga tu ya kufa mtu, yaani kama huna simile utapatwa na aibu ya mfadhaiko yaani jinsi Wema anavyonyonga kiuno mmh... Acheni Diamond adate wajameni.
Makao Makuu: Aaa Mateja acha hizo hebu nidokeze na kinachoendelea hapo Serena Hotel?
Mateja: Mkuu huku mambo yameshamiri, namuona Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen anaingia ukumbini huku akijiburuza na magongo.

Makao Makuu: Magongo! Amepatwa na swaibu gani tena?
Mateja: Hata mi sijapata uhakika sema kuna jamaa kaninong’oneza kuwa eti naniliu wake kamnaniliu lakini ntakwambia vizuri kesho.

Makao Makuu: Nini kingine kinaendelea hapo?
Mateja: Mkuu Mzee Majuto amepewa tuzo na sasa amefurahi sana na anawaalika watu kwenye msiba wake, anaomba siku akifa watu waje kwa wingi kwenye mazishi yake.
Makao Makuu: Dah! Huyo mzee haishi vituko nani wengine wamepata tuzo?
Mateja: Wengine ni Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Salama Jabir, Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Salim Kikeke wa BBC Swahili na wengineo.

Makao Makuu: Sawa Mateja angalia matukio kumbuka kupiga picha nitakusaka baadaye.   
Saa 5:12 usiku
NJEMBA YADATISHWA NA VIUNO VYA BIBI BOMBA
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Bukos)

Bukos: Yaa mkuu wangu, nakupata kijana wako niko kwenye Bar moja inaitwa Madoto huku Mburahati nilikuwa nafuatilia Shindano la Bibi Bomba si unajua leo ilikuwa ndiyo fainali?
Makao Makuu: Nini kinaendelea huko uswazi kwa wanaofuatilia fainali hiyo kwenye runinga?
Bukos : Mkuu kuna muda Five Stars Modern Taarab walikuwa wakirindimisha burudani huyu Bibi Bomba, Ruth Manfred a.k.a Weusi Hawana Kwele, alikata nyonga mpaka akaenda chini kuna mlevi mmoja huku akajifanya eti amezidiwa baada ya kudatishwa na nyonga za bibi huyo kajitapa eti ni lazima atafute namba yake.

Makao Makuu: Dah! Hivi ni wangapi wameingia fainali?
Bukos: Mkuu fainali ya leo waliingia wabibi watano, Mariam Ligaya ‘Mamaa wa Mji Kasoro Bahari’, Anastazia Chambo, Ruth Manfred ‘Weusi Hawana Kwele’, Sofia Shomari na  Sulaiya Mohammed ‘Agwe Solowenyo’.

Makao Makuu: Vipi nani kachukua hizo milioni 13 walizotangaziwa?
Bukos: Mkuu mpaka hatua ya mwisho walibaki wawili, Mariam Ligaya wa Moro na Ruth Manfred na Ruth Manfred ndiye kaibuka mshindi hivyo anakabidhiwa milioni 10 na zile milioni 3 ataongezewa milioni 2 na kupewa kiwanja Kigamboni chenye thamani ya shilingi milioni 5.

Saa 6:57 usiku
MOSHI WA GANJA WATIBUA SHOO YA MIAKA 10 YA MKALI WA RHYMES MORO
Makao Makuu: (Mkuu anamtwangia Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’) Halooo halooo Mkude Simba...
Shekidele: Nakupata Mkuu.

Makao Makuu: Haya niambie muda huu uko wapi?
Shekidele: Mkuu wangu niko katika Ukumbi wa Terminal Pub hapa Msamvu,  Mkali wa Rhymes, Afande Sele na washirika wake wanapiga shoo ya kusherehekea miaka 10 ya kushikilia taji la mkali wa rhymes.
Makao Makuu: Ahaaa... vipi hali ikoje?

Shekidele: Mkuu mpaka mida hii, 20 Percent na Afande Sele mwenyewe wameshakamua tatizo alipotaka kupanda O-Ten ameshindwa kupiga shoo baada ya kuzidiwa na mambo fulani maana kwa muda mrefu nilikuwa nikimuona akipiga maji huku akila kuku moshi.
Makao Makuu: Nini kinaendelea sasa?

Shekidele: Mkuu onesho naona kama limevurugika maana mambo sasa ni vululuvululu, moshi umetawala ukumbini wengine wasiouzoea wanakohoa hovyo hata mimi hivi ninavyoongea nimeshindwa kuvumilia hali ya ndani niko nje ya ukumbi, yaani ukumbini watu macho mekundu kama wamemwagiwa unga wa pilipili.
Makao Makuu: Sawa Mkude Simba ukitoka hapo wapigie wenzako waambie mkapumzike.
Shekidele: Pouwa Mkuu.
Read more >>

MZEE MAJUTO AFUNGUA, BAADA YA KUKAA KWA MUDA MREFU, SOMA ALICHOKISEMA HAPA

KingMajutoMchekeshaji  wa  muda  mrefu  Amri  Athuman  ‘Mzee  Majuto’  ametoa  kali  ya  mwaka  baada  ya  kusema  kuwa  maisha  yake  ni  komedi  tosha  kutokana  na  kumvunja  mtu  mbavu bila  kujali  yuko  mahala  gani….
 

JANGA JINGINE KWA MBASHA: ALIZWA HATI ZA NYUMBA, VIWANJA

Akizungumza  na  mwandishi  wetu, Mzee  Majuto alisema  yeye  hutoa  shoo  muda  wowote  bure   bila  kujali  yuko  katika  wakati  gani   kwani  maisha  yake  ni  komedi  tupu…
 
“Maisha  yangu  ni  komedi  tosha,siwezi  kuacha  kuchekesha.Wakati  mwingine  si  kwa  kupenda  bali  huwa  najikuta  tu  nimefanya  hivyo ,  inabidi  watu  wanizoee  tu….
 
“Huwa  sina  nia  ya  moja  kwa  moja  kuchekesha  watu, lakini  kumbe  kauli  zangu  huwavunja  mbavu.Sijisikii  vibaya  kwa  hilo, najivunia  kuendelea  kuwa  msanii  ninayekubalika  hadi  umri  huu,”  alisema  mzee  Majuto
 
Read more >>

MFAHAMU KING MAJUTO KWA KUSOMA HISTORIA YAKE NA KUJUA FILAMU KALI ALIZOZICHEZA HAPA

tanzania-king-majuto

Amri Athuman’ King Majuto’  alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majato ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.
Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
NA HIZI NDIZO MOVIE ALIZOCHEZA KING MAJUTO, PIA UNAWEZA KUBONYEZA KILA JINA LA MOVIE NA UKANUNUA ONLINE.
·         Ndoa ya Utata |
·         Daladala |
·         Nimekuchoka |
·         Mbegu |
·         Zebra |
·         Shikamoo Mzee |
·         Tabia |
·         Utani |
·         Tikisa |
·         Trouble Maker |
·         Gundu |
·         Kizungunguzu |
·         Shoe Shine |
·         Street Girl |
·         Faithful |
·         Mtego wa Panya |
·         Boss |
·         Back with Tears |
·         Sikukuu ya Wajinga |
·         Nyumba Nne |
·         Chips Kuku |
·         Kitu Bomba |
·         Ndoto ya Tamaa |
·         Lakuchumpa |
·         ATM |
·         Bishoo |
·         Tupo Wangapi |
·         Moto Bati |
·         Varangati |
·         Out Side |
·         Pusi na Paku |
·         Juu kwa Juu |
·         Swagger |
·         Oh Mama |
·         Jazba |
·         Mke wa Mtu Sumu |
·         Mbugila |
·         Kidumu |
·         Mkali Mo |
·         Mpela Mpela |
·         Utanibeba |
·         Babatan |
·         Mjomba |
·         Msela wa Manzese |
·         Karaha |
·         Mpango Sio Matumizi |
·         Mume Bwege |
·         Shuga Mammy |
·         Embe Dodo |
·         Nakwenda Kwa Mwanangu |
·         Seaman |
·         Naja Leo Naondoka Leo Tanga |
·         Mgeni Njoo |
·         Kuwadi |
·         Kulipa Tabu |
·         Uso wa Mbuzi |
·         Machimbo |
·         Fundi Feni |
·         Mwizi wa Kuku |
·         Mtu Mzima Hovyo |
·         Vituko Show Vol. 10 |
·         Bettery Low |
·         Brothers |
·         Alosto |
·         Back from New York |
·         Kipofu |
·         Koziman Vol 21 |
·         After Money |
·         Talaka Yangu |
·         Gereji |
·         Welcome Back |
·         Mshamba |
·         Pedeshee |
·         Waiter |
·         Inye Plus |
·         Inye Gwedegwede |
·         Inye Vol.1 |


Source: Mdadisi Mambo Blog
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger