Showing posts with label ALLY KIBA. Show all posts
Showing posts with label ALLY KIBA. Show all posts

ALI KIBA AFUNGUKA MANENO MAZITO KUHUSU BIFU LAKE NA DIAMOND


Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na

tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu
waache kuwakosanisha.
Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka
watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha
Diamond ili wafanye muziki mzuri.
“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na
Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake
za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema
kuna wengine wanafanya for fun na wengine
wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya
lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba. “Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali
waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu
mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina
mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport
kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi
ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania.
Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili
tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi
wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye
kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani
ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.
Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia
mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso
pamoja na ujio wa video zake. “Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama
nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani
yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika
kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu
wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe
zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya
kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha.
Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo
tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla
sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni
hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema
nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa
track mbili moja itafanyika hapa na nyingine
itafanyika nje.”
Read more >>

BABU TALE AFUNGUKA KUHUSU ALI KIBA KUMZIMA DIAMOND.

 
Meneja wa Diamond, Babu Tale amezungumzia kile kile kinachoelezwa kuwa ni beef kali ama ushindani mkubwa kati ya Diamond na Ali Kiba, moja kati ya mada ambazo zinatengeneza mijadal mingi sana kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Times Fm, Babu Tale amejibu swali la msikilizaji aliyetaka kufahamu mtazamo wake kuhusu uwepo wa beef kati ya wasanii hao wawili.

“Mimi sidhani kama Diamond na Ali Kiba wana beef, ni biashara…challenging. Sijawahi kuona wanagombana katika maisha yangu. Watu wanaoandika nyuma wanaandika kwa sababu wanaamua kuandika lakini mwisho wa siku Diamond na Ali Kiba wote ni wanamuziki. Without challenge Diamond hawezi kuendelea au Ali Kiba hawezi kuendelea.” Amesema Babu Tale.
Ameeleza kuwa hiyo kwake anaona challenge hiyo ni nzuri kibiashara na sio tatizo na kwamba likionekana ni tatizo watalitatua.

“Kama unamfollow Davido na Wizkid. Kila anapopost Wizkid kwamba hapa nafanya show hivi, Davido nae anamjibu kuwa angalia watu wamejaa huku hivi. Ni biashara. Ugomvi wanagombania nini? Ali Kiba anakula kwale ana maisha yake, Diamond anakula kwake na ana maisha yake.” Ameongeza Babu Tale.

Alipoulizwa kuhusu ujio wa Ali Kiba kuchukuliwa kama ndio sehemu ya mapinduzi dhidi ya utawala wa Diamond, Babu Tale aliipinga kauli hiyo.

“Huwezi kusema Ali Kiba anakuja, Ali Kiba yupo na alikuwepo. Huwezi kumuambia anakuja unamdhalilisha, Ali Kiba yupo alikuwepo na ana uwezo wake. Anafahamu base yake. Huwezi kumwambia anakuja, anakuja ni msanii mpya…Raymond wa Tip Top anakuja sio Ali Kiba. Usiwe na mind kuwa Ali Kiba hayupo kwenye Game, yupo.” Ameongeza kuwa hajafirikia kuhusu suala la Ali Kiba kumpindua Diamond.
Read more >>

RIPOTI KAMILI KUHUSU WIMBO WA ALI KIBA, 'MWANA' NA 'MDOGO MDOGO' YA DIAMOND.

July 25, mwaka huu, Ali Kiba alivunja ukimya wa muda mrefu kwa kuachia nyimbo mbili kwa mpigo ambazo ni ‘Mwana Dar es Salaam na Kimasomaso’. Wengi walisubiri kwa hamu ujio wake mpya na waone kama kweli atatusua au itabuma!

Bila shaka yeye pia alikuwa na tension kujua jinsi gani nyimbo hizo zitakavyopokelewa na mashabiki hao. Je wazikubali sana au wataona kawaangusha?
Ripoti zilizonaswa na tovuti ya Times Fm kupitia vyanzo mbalimbali vikiwa ni pamoja na baadhi ya ma DJ wanaofanya kazi Times Fm Radio na katika club mbalimbali zinaonesha kuwa Mwana Dar es Salaam inafanya vizuri sana hasa club.
“Aisee, kwa kweli nimepiga club kadhaa na kuhudhuria club karibia zote kubwa za mjini. Nimegundua wimbo wa Ali Kiba, Mwana Dar es Salaam unafanya vizuri sana. Kiukweli inafanya vizuri sana hasa kwa kulinganisha na muda ulioingia sokoni. Yaani ukiupiga unaona watu wanakuelewa kibao aisee.” DJ ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia tovuti ya Times Fm.
DJ mwingine ambaye alikubaliana na maelezo ya DJ wa kwanza kuhusu wimbo wa Ali Kiba, aliongeza kuwa bado wimbo wa Diamond, Mdogo Mdogo ndio wimbo ambao anaweza kuutaja kama wimbo wa kuwaamsha watu zaidi.
“Ukitaka club pavurugike. Yaani watu wafurike kwenye dance floor kwa fujo… we piga tu MdogoMdogo ya Diamond. Yaani haielezeki shangwe yake aisee. Watu wanapagawa.” Alisema.
Nyimbo zote mbili zinapata nafasi nzuri sana katika vituo vya radio. MdogoMdogo ambayo ina video ya kimataifa inachezwa sana na kukubalika kwenye vituo vya mbalimbali vya runinga. Youtube, video hiyo imeshaangaliwa zaidi ya mara 717,000 kwenye akaunti ya Diamond pekee.
Mashabiki wengi wana kiu ya kuiona video ya wimbo wa Ali Kiba ambayo inabidi iwe na level kubwa kulingana na wimbo wenyewe.
Wimbo wa Diamond ‘Mdogo Mdogo’ ulitoka rasmi June 12, baada ya mwezi mmoja na wiki moja ukatoka wimbo wa Ali Kiba ‘Mwana Dar es Salaam’.
Read more >>

ALLY KIBA ATOA MAJIBU KWA NINI KAFUTA FOLLOWERS WAKE, HABARI KAMILI HAPA

Baada ya kutupiwa lawana nyingi na maswali yakiendela kumiminika ili atoe sababu ya kuunfollow watu kwenye mtandao wa Instagram hatimaye msanii Ali Kiba ameamua kujibu kama ifuatavyo:



  Hapo juu ni swali kutoka kwa mtangazaji wa Times FM Fadhili Haule na fans wengine
Hili ndo jibu la Ali Kiba. So ukitaka kuwasiliana nae tanya kumfollow twitter.
Read more >>

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA ZAIDI BIFU LAKE NA ALI KIBA!

Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita baridi.
Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya habari.
Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti anaouona kati ya wasanii hao. 
 
Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana hazina kubwa ya sauti na anakumbuka kuwa Diamond aliwahi kuisifia.
“Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi.” Amesema G-Lover.
Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho Diamond anakifanya sasa hivi.Lakini unapokuja kibiashara Diamond huwa anazungumza kuwa yeye muziki wake anaufanya kibiashara na ndo maana ana team work kubwa ambayo inamsaidia yeye kujua ni kitu gani anatakiwa kufanya, kuna kitu gani anatakiwa kukifanya kwa upande wa muziki.  
Sasa kwa upande wa Ali kwa sasa hivi, kwa kipindi niko naye nilikuwa na team ambayo hata yeye alikuwa hajui mimi nipo na akina nani nyuma yangu. Alikuwa anajua kuwa yupo G, lakini nyuma yangu nilikuwa na watu takriban thelathini ambao ni team work ambayo ilikuwa inafanya kazi kwa Ali Kiba kujua ni kitu gani na kitu gani tunatakiwa tufanye ili afike na mpaka akafika hapo. Ameeleza.
 
“Diamond naye anafanya vitu kama hivyo, unaweza kuona Diamond ana team ya watu watatu tu au wanne ambao wanamsaidia, kwahiyo utaona Diamond kuna watu kibao ambao amewapa ajira. Kwahiyo Diamond hawezi kuwaangusha watu ambao wapo nyuma yake ambao wamepata ajira kutoka kwake. Kwa mfano kuna utofauti mkubwa ambao Diamond amekuja nao ambao ukiangalia ni utaratibu uleule ambao nilikuwa nikiufanya kwa Ali. Kwahiyo sijui kuna utofauti gani kati ya management ya Diamond na ya Ally Kiba ya sasa hivi
Read more >>

ALI KIBA ASEMA, LULU ANAFAA KUWA MKE

HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba ndani ya ofisi za global.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.

AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akiwa na Ali Kiba.
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?

Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke. Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa? Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.

'Kanumba The Great' enzi za uhaim wake.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.

“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.

KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.

KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.

“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu  wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.

“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi wetu ili  azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta ili afunguke).
Read more >>

BIFU LA ALLY KIBA NA DIAMOND SASA LAFIKIA PABAYA SANA, ISHU NZIMA IKO HAPA



Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
  Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:
“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema mimi ndiyo nilimfuta.
 
Staa wa muziki Bongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.
“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye alitengeneza ule wimbo.
 
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu'
“Sikuwahi kwenda studio na Diamond, sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).
Nikamwambia itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo wake, shahidi prodyuza wangu KGT.
 
“Kutoka hapo nikaona hakuna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri. “Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.
“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” Baada ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu.”
Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo bado ni mbichi.
Read more >>

UKWELI JUU YA CHANZO CHA BIFU KUBWA KATI YA DIAMOND PLATNUMZ NA ALLY KIBA, SOMA UKWELI HUOA HAPA


Leo ilikuwa ni siku ya Ya mkali wa zamni wa Bongo fleva, Ali kiba akiachia ngoma zake mbili katika kipindi cha XXL cha CLOUDs FM, Kama umefuatilia katika wiki hii kumekuwa na vuguvugu kali linaloendelea kati ya Mahasimu hawa wawili, sasa wengi wakiwa hawajui nini chanzo cha Bifu kubwa linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba.

Katika ali ya kutaka kujua ukweli mtangazaji wa kipindi hicho alimtandika swali la kizushi Ali Kiba kuhusu Bifu hilo linaloendelea mapka sasa huku akitaka kujua chanzo kikubwa cha yeye na Diamond na yeye kuhitiliafiana. Ali aligoma kabisa kuelezea chanzo cha ugomvi ama bifu lililo kati yao. 
Bila ajizi Dj FETTY aliamua kuweka wazi chanzo cha vuguvugu hilo. kuwa katika wimbo wa LALA SALAMA wa Diamond kulikuwa kuna mistari ama verse ambazo alitakiwa kuimba Ali Kiba, lakini kwa mshangao Diamond alifuata mistari ambayo Ali Kiba ilibidi aimbe, na kwa upande wa pili Alikiba katika wimbo wake wa Single boy pia kulikuwa kuna verse ambazo Diamond ilibidi aimbe lakini Alikiba akaamua Kumtolea nje na kumshirikissha Lady Jay dee.

Kwa hiyo Hiyo no sababu kuu kati yanyingi zinazopelekea Bifu kubwa kati ya wasanii hawa wawili wa Bongo Fleva. ni mengi yamezungunzwa ndani ya kipindi hicho cha XXL
Read more >>

ALLY KIBA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU BIFU LAKE NA DIAMOND


STAA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Alikiba amekanusha kwamba ana ugomvi na nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ kama ilivyokuwa ikifahamika na wadau wengi wa muziki huo.
Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show kinachorushwa na Clouds TV, alisema hana ugomvi na msanii yeyote kwani anajitambua na hawezi kuendeleza chuki na wasanii wenzie.
Diamond aliwahi kunikosea sana, lakini mimi kwa sababu sio mtu wa kukasirikika niliamua kuachana nae na kufanya yangu, lakini nashangaa kila kukicha nasoma kwenye vyombo vya habari kwamba nilimkosea, lakini kiukweli sina ugomvi na mtu.
Katika wimbo wake wa ‘Lala salama’,
Read more >>

BIFU LA DIAMOND NA ALLY KIBA LACHOCHEWA NA OMMY DIMPOZ, SOMA ZAIDI HAPA

ommy
Kwa Kile Kinachoonekana kuwa kuna Beef kati ya Diamond na Ali Kiba ya Kimuziki , Baada ya Ali Kiba Kuojiwa na Kusema Kuwa hata Kaa Aongee na Diamond..Diamond Ameandika Kwenye Insta Maneno Ambayo yanaonekana ni Jibu lake kwa Ali Kiba, Mchana huu tena Ommy dimpoz amepost Picha hizo apo chini na Kuandika (Siku Mashabiki wa Ali Kiba na Diamond) akiashiria kuingila Ugomvi ama Bifu linaloendelea kati ya mahasimu hawa wawili,. Sasa swali ni je Ugomvi huu Ommy unamhusu vipi au ndio kuchochea ugomvi badala ya Kuhusuluisha… Wacha Movie Iendeleeeee
Ommy Amemaanisha kuwa hapo ndio itakavyokuwa siku mashabiki wa Diamond na Ali Kiba watakapokutana 
Read more >>

BAADA YA SENTENSI ZA ALLY KIBA, DIAMOND AMJIBU MANENO YENYE KUMDHALILISHA ALLY KIBA, YASOME HAPA MWENYEWE

diamondWiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii zilitoka stori ambazo zilizanzia kwenye 255 ya Clouds Fm ambapo aliulizwa Ally Kiba juu ya uhusiano na msanii mwenzake Diamond Platnumz.
Usiku wa kuamkia July 21 Diamond Platnumz ameandika ujumbe ambao mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva wameutafsiri kama majibu juu ya kile alichokisema Ally Kiba wiki iliyopita.
Katika ujumbe huo ambao Diamond kapost kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kaandika>>’Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke,Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu’.
Usisahau kulike page yetu ya Utamu wa mapenzi hapa<<UTAMU WA MAPENZI>>
dimaond
Read more >>

ALIKIBA NA DIAMOND..UNAAMBIWA KUJA KUTOKEA TENA KAMA MAAJABU YA DUNIA

Wazungu wanasema picha huongea maneno elfu moja, hii ni kabla Diamond hajanza kugeuka kuwa sukari ya warembo na wakati huo Kiba ndio akiwa ndio talk of the town, hapa ni kabla hata mambo ya mabifu hayakuwepo, wakati mambo yalikuwa shwari kabisa...
Ila kwa hivi sasa bado ni ndoto kupata picha kama hii wawili hawa wakiwa pamoja...
Read more >>

SABABU ZA ALI KIBA KUFELI KUMUZIKI, SOMA HAPA


Katika segment ya KITENGO, leo katika Kipindi cha Planet Bongo Kinachorushwa EATV: Host Abdallah Ambua Alimtembelea Msanii Wa Muziki wa B'flava, Ally Salehe Kiba, nyumbani kwao anapoishi yeye na familia yake kwa ujumla::Nilikuwa na shauku ya kusikia nini ambacho Ally K angekizungumza kuhusiana na Muziki wake kwa ujumla na hii ''Backwardness'' yake licha ya kuwa msanii mkubwa na anayependwa zaidi Bongo;

After Interview Nilijifunza vitu vifuatavyo:

Kitu cha kwanza ambacho kilinishtua ni Kuona Setup ya Location ambayo waliichagua kufanyia Interview, Lazima niseme wazi haikuwa Kwa Hadhi yake - Hata kama ni usimple, that was too much...
Kwa ufupi ilikuwa ni Unprofessional !! Walikaa on a rough and shabby set mpaka nikawa naichungulia mara mbili mbili.

Kingine ni the way anavyojichukulia: Ni mtu ambae anaonesha kama ndoto zake zote kimuziki zimeshatimia, Especially kufanya kazi na msanii mkubwa duniani , R kelly: He sounded like Nani kama mimi in Tz... HAKUNA !Pia; Namna alivyokuwa anazungumza na kujibu maswali, Haonekani kuwa na strategy zozote za kuukuza Muziki wake na kufanya kitu ambacho mashabiki wake wengi wanakitarajia Aidha ni kwa kutopenda kuanika mambo yake (maybe) lakini as an artist hakuwa na ile promising attitude..

Mengineyo: Hakuvaa vizuri, Hakuwa na ile starlook kabisa, He looked more of An Undergroundartist:

My Take: Inakatisha tamaa kuwa mshabiki wa msanii ambae hana hata dalili za kukata kiu yako kama mshabiki. Ni kwa vile anajua kwamba we are addicted to his music au ni nini?

Ifikie hatua mshkaji ajiongeze kidogo, Music is Business, Na luckily he's on a high demand, Ningefurahi kama angejikagua tena na kufanya kitu ambacho shabiki zake wanapenda.Nisingependa kumtaja; Lakini Diamond is a nice mirror to look at : Sio dhambi Kuiga vitu vizuri.
NAISAPOTI..................... .......

#BringBackOurArtistCampaigne
#ALLYKIBA
Read more >>

ALIKIBA SASA KUWASAHAULISHA MACHUNGU WABONGO, HII NIBAADA YA DIAMOND KUKOSA TUZO MTV MAMA,

DSCN0027
Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba hivi karibuni wanatarajiwa kuwasahaulisha wabongo na story zote za mtv mama, na kuhusu yote yaliyojiri kwa kuwaletea bonge la show litakalofanyika pale new maisha club jumapili hii.Huu ni ujio mpya wa Alikiba baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuonekana hata kwenye media mbali mbali za hapa bongo, jambo lilowafanya baadhi ya fans wa Alikiba na muziki wa bongo fleva kwa ujumla, kujiuliza kama mkali huyu amepotezea muziki au la. Habari zilizo chini ya kapeti zinasema kuwa kiba yuko chimbo sasa hivi akijipanga kwa ujio wake mpya kabisa, na sasa hivi anapasha tu kwa makubwa aliyoandaa kipindi chote alichopotea kwa muda.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger