Showing posts with label JB. Show all posts
Showing posts with label JB. Show all posts

RAY, JB WAMPIGIA SALUTI KAJALA, KISA KIZIMA HIKI HAPA

Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti muigizaji mwenzao,  Kajala Masanja kutokana na filamu fupi aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na waandishi wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa  Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.
Kajala Masanja akiwa na mwanaye, Paula.
“Kitu ambacho nimekipenda ni kwamba filamu ni fupi lakini ujumbe umeeleweka pia amefikiri kitu cha tofauti kabisa kwani hata watoto wa rika zote wanaweza kuangalia kwa ajili ya kujifunza,” alisema JB huku Ray akiunga mkono hoja.
Read more >>

JB AJITAPA KUWA STRAIKA, MCHEKI HAPA

TAMBO! Bonge la Bwana, Jacob Steven ‘JB’ amejitapa kuwa licha ya mwili wake kutoonekana wa mazoezi lakini yeye ni bonge la straika.
Bonge la Bwana, Jacob Steven ‘JB’.
Akistorisha na paparazi wetu, JB ambaye anatamba na filamu ya Shikamoo Mzee, alisema mpira alianza kucheza kitambo tangu alipokuwa akiichezea timu ya JKT Mgambo na Mutukula ya Mwananyamala Dar hadi sasa kwenye Klabu ya Bongo Movie wanamtegemea.
‘JB’ akiwa mazoezini.
“Kwenye mambo ya mpira mimi ni noma, ni bonge la straika, Bongo Movie wananitegemea, watu wasinichukulie poa niko fiti sana kimazoezi,” alisema JB.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger