Showing posts with label UWOYA. Show all posts
Showing posts with label UWOYA. Show all posts

HIZI NDIZO PICHA ZA UTATA ZA UWOYA...NI BALAAA

Hizi picha za msanii uwoya zimekua ni gumzo sana mtandaoni, tazama jinsi anavyojiachia bila kujali.
Read more >>

JOHARI AMCHANA IRENE UWOYA, PIA AWACHANA WAIGIZAJI WA KIKE WANAOJICHIA NA KUPOTEZA MVUTO

Msanii  Johari Blandina ‘Chagula’ ambaye ni star mkongwe Swahiliwood amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuutunza muonekanio wake na kuwa kama kijana licha ya umri wake kuwa mkubwa tofauti na baadhi ya waigizaji wenzake wa kike ambao hujiachia na kuonekana wazee licha ya umri wao kuwa mdogo.

Akizungumza na Filamucentral Johari alisema:

“Wasanii wa kike wengi ni watoto wadogo lakini kwa sababu ya kujiachia wanaonekana kama watu wazima lakini ukweli ni watoto wadogo sana, namshukru Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini mwili wangu upo fiti,”
 
Johari alimtolea mfano Irene Uwoya ambaye ni shoga’ke wa karibu kuwa anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya kujiachia licha ya kwamba amempita miaka kadhaa. 
johari
 
Vile vile Johari amesema kuwa kawasasa amerudi kwa moto wa kasi kama muigizaji kama awali baada ya kuwa upande wa producer kuwapa nafasi chipukizi ambao wengi amesema wameshindwa, hivyo amerudi mwenyewe kwenye game.
Read more >>

IRENE UWOYA "SIPENDI KUVAA NGUO ZA NDANI NA SINA KABISA KABATINI"


Mrembo na staa wa filamu nchini Irene Uwoya amesema kuwa hakuna vazi asilolipenda kulivaa kama chupi a.k.a kufuli. Irene amesema hayo alipokuwa akizungumza na
magazine ya burudani ya VIBE.
Alipoulizwa na mwandishi wa jarida hilo kuwa ni nguo gani ni vigumu kuikuta kwenye kabati lake, “Chupi – sipendi kabisa hilo vazi” Alisema Irene uwoya. Hatari sana hii.
Read more >>

UWOYA AMUONYESHA HONEY WAKE NA KUPIGA PICHA ZA MIKAO TATA, SHUHUDIA MWENYEWE HAPA

Msanii kutoka Tanzania House of Talent Msami Giovanni ambaye kwa wakati huu ana hit na ngoma yake ya Sound Track kwa wakati huu inasemekana eti yuko katika dimbwi zito la mahaba na muigizaji maarufu wa 
Bongo Movie Irene Uwoya
,
Gazeti La Makorokocho lilimtafuta Msami na kumuuliza ukweli juu ya Taarifa hizi lakini alichomoa, sikuishia hapo nikamtafuta Girl friend wake wa zamani au niseme ambaye wamegombana kutokana na Msami kuchepukia kwa Uwoya,
Girl Friend huyo anayeitwa Rehema ambaye pia ni Dancer mkali sana maarufu akatiririka kuwa ni kweli taarifa hizo anazo ila ana uhakika Msami atarudi kwake wala hana Wivu na Uwoya na anachofahamu Irene Uwoya eti alimlaghai Msami kwa kumwambia eti anataka kuwa meneja wake kwa kuusimamia muziki wa Msami, sasa tangia hapo wawili hao wakazama kwenye Dimbwi zito la mahaba
widgets for blogger
Read more >>

UWOYA AFANYA FUJO KUBWA NYUMBANI KWA MUME WA MTU

NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena! Safari hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake (jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘nyumba ndogo’. 
Nyota wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba, siku ya tukio, Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake (hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo, Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa, mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza, kwa hiyo yeye aliye tu!

UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa! Alianza kusema maneno ya kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio. Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi.

“Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo mke mpya,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.
Nyumba anayodaiwa kufanya fujo
AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza kuishia polisi, Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni, Dar ambapo alifanya fujo.

“Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi,” chanzo kilisema.
HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa, Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘kujaza nzi’ (watu kuwa wengi) ambapo aliondoka mdogomdogo na kama hana hasira utadhani si yeye aliyekuwa akichafua hali ya hewa.

MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa, Irene alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kwenda halijojo!

“Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu,” kilisema chanzo.
ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘nyumba ndogo’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo.

UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba, alishaachana na mwanaume huyo.

“Ilitokea, lakini nilishaachana naye. Unajua ishu si kwamba angenioa mimi, ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana,” alisema Uwoya.
AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa, msanii huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la!
Uwoya: “We niache tu, nina mambo mengi sana yanayoniliza mimi.”
Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu.” Kisha akakata simu.

HISTORIA
Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa Julai 11, 2009 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Mei 8, 2011 walijaliwa kupata mtoto wa kiume aitwaye Krish.
Hata hivyo, Novemba 16, 2011 kwenye gazeti hili kuliandikwa habari yenye kichwa;

NDOA YA UWOYA YAVUNJIKA.
Ndoa hiyo iliparaganyika baada ya Uwoya kudaiwa kumkataa mwanaume huyo na mpaka sasa haijasimama tena huku mwanaume akiwa kwao, Rwanda.
Read more >>

HIVI KUNA NINI HADI UWOYA NA MASOGANGE WANAISHI PAMOJA SOUTH

Hili ni swala la kujiuliza...ingawa hadi sasa Uwoya hajasema chochote...Lakini Masogange kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM amekuwa akiweka picha kadhaa za Irene Uwoya wakiwa pamoja huko SAUZI....Sasa katika kumaliza zaidi jana ameka video Irene akiwa anapika....HEHEHEHE
Read more >>

UWOYA SASA AHAMISHIA PENZI KWA MSANII JAGUAR

Latest news say that the star of the film has met Irene Uwoya privacy Nairobi, Kenya and another star in the country music from Jaguar. One source that is close to Uwoya Speaking to   said it that the couple is no deal they consider working together but not sure 
until now is deal would "Uwoya and Jaguar have met privately no issue their sons-talk but do not know how deal do these, I will give updates" said a source the last

However, another source from Kenya has undertaken that did you see Uwoya and Jaguar in a hotel in Nairobi while in session zero distance romantic aka "Hi, I have seen Irene Uwoya with Jaguar in a hotel in Nairobi THEY looked like an item, these celebs are not predicted "said the source 

Mhariri has tried pageant Uwoya but his phone was not found, however recently laid Uwoya picture at Julius Nyerere International Airport to Nairobi saying he did not make it clear as though going to work or not! . Tunamsaka Uwoya to afunguke own live
Read more >>

HAWA NDIO MASTAA WA KIBONGO WANAOMEGWA NA WANAUME WENYE UMRI MDOGO, WEMA NDIO KIONGOZI, SHILOLE ANAFUATA

ms
Mara nyingi tunaishia kusikia rumors tu, kuwa msanii fulani amemzidi umri mpenzi wake na mara nyingi mwisho wa siku rumors zinabaki rumors tu, hadi pale wawili watakapofunguka wenyewe juu ya suala hilo, basi hii ni list ya wasanii wachache tu maarufu na wenye majina hapa town, ambayo inasemekana kuwa wamepigana gape kiumri.
 
Diamond Platnumz Vs Wema Sepetu.
 
Kutokana na wikipedia Diamond Platnumz amezaliwa mwaka 1989 wakati Wema Sepetu amezaliwa mwaka 1988,  wawili hawa walioshibana wamepishana miezi michache tu, huku Wema Sepetu ndio inaonyesha amemuacha Diamond Platnumz kwa miezi michache tu. Hii ni moja ya couple maarufu sana Africa, huku kila mmoja akiwa ana-shine bila kutegemea mgongo wa mwenzie, Diamond akiwa anakimbiza kwenye anga za muziki wakati Wema akiwa ndio actress maarufu anayependwa zaidi na watu na anayeongoza kuwa na mashabiki wengi East Africa.
 
Shilole Vs Nuh Mziwanda.
 http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/mzuwanda1.jpg?resize=430%2C430
Rumors had it kuwa Shilole amempiga gape(amemuacha kiumri) Nuh Mziwanda, na siku ilipofika wawili hao walipoamua kufunguka juu ya mapenzi yao, story zilizagaa kuwa Shilole amepata serengeti boy, ingawa hadi hivi sasa haijulikani wameachana kiumri kwa miezi au miaka mingapi.
Irene Uwoya Vs Msami.
 
Ni juzi kati tu, wadau walibaini kuwa wawili hawa wapo katika mapenzi moto moto, na mwisho wa siku ikabidi wafunguke na ku-confirm ukweli huo kuwa wao ni wapenzi kwa sasa, ila rumors had it kuwa Irene Uwoya amemzidi umri Msami, na watu kuanza kuamini rumors hizo hadi pale Msami juzi kati alipoamua kufunguka kuwa yeye amemzidi umri Uwoya kwa miezi mingi tu, ingawa hakufunguka kuhusiana na miezi mingapi.
Read more >>

HUYU NDIO MTOTO WA KIUME WA MSANII BONGO MOVIE IRENE UWOYA, HE IS SO HANDSOME

Ama kweli watoto hawachelewi kabisa kukua, huyu ni motto wa superstaa wa bongo movie Irene Uwoya, motto huyu anaitwa krish inapendeza sana toto la ukweli, hongera sana Irene mwenyezi mungu akukuzie mwanao 
Read more >>

UWOYA NA BEBI WAKE NI KULALA MZUNGU WANNE, SOMA KILA KITU HAPA

Msanii wa muziki wa bongo flava Msami amemkana kiaina mrembo na msanii wa bongo movie Irene Uwoya akitia ugumu kukubali moja kwa moja kama ni wapenzi.

Msami katika mahojiano na Mamu Africa Blog alikuwa mgumu kukubali moja kwa moja kama wana mahusiano ya mapenzi na Uwoya akisisitiza kuwa mrembo huyo ni zaidi ya rafiki.

Akaenda mbali zaidi akisema mara kadhaa amekuwa analala na Uwoya kitanda kimoja hata siku mbili mpaka tatu lakini wanalala mzungu wa nne.

"Unajua Uwoya ni best friend wangu sana sana,wakati mwingine nakwenda kwake tunapiga stori mpaka usiku,tunaangusha pamoja hata siku mbili tatu kitanda kimoja lakini huwa tunalala mzungu wa nne tu" alisema Msami.

Msami aliendelea kuzunguka kuukubali akitumia neno kwa mfano kama ni wapenzi na Uwoya kukutana kwao ni baada ya kazi zao kwakuwa kila mmoja ana majukumu yake ya kikazi.

"Unajua kwa mfano tuna imagine kuwa Uwoya ni mpenzi wangu,mara nyingi tunakutana baada ya mihangaiko yetu ya kila siku.

Baada ya danadana za hapa na pale na kubanwa hatimaye Msami akakiri kuwa kweli anatoka kimapenzi na Uwoya.

Aidha Msami amesema anashangaa watu wanaosema kuwa Uwoya anatoka na Serengeti boy wakati hawaujui ukweli wa jambo hilo,kwakuwa yeye ana umri mkubwa zaidi ya mrembo huyo.

Amesema amemzidi Uwoya kwa kuzaliwa kwa miezi kadhaa kwahiyo yeye sio Serengeti boy kwakuwa ni mkubwa kwake.

"Nawashangaa watu wanasema eti Uwoya anatoka na Serengeti Boy yaani hata ukweli hawaujui mimi ni mkubwa nimemzidi miezi kadhaa wanasemaje eti ni Serengeti Boy waache hizo" Msami alisema.
Read more >>

UWOYA AFUNGUKA JUU YA PENZI LAKE NA MSAMI: NAMPA MSAMI KILA KITU,

Jana May 28 kupitia You heard ya XXL Clouds FM ilikua ni stori kuhusu uhusiano wa Msami wa THT na mwigizaji toka Bongo Movie Irene Uwoya na jana alisikika Msami ambaye alikanusha uhusiano lakini mpenzi wake Rehema aliweka wazi kuwa ni kweli Msami ana uhusiano wa kimapenzi na Irene Uwoya.

Sasa May 29 2014 ishu hii imeendela ambapo katafutwa Irene Uwoya na kuulizwa na Soudy Brown kama ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Msami na swali la kwanza lilitaka kujua uhusiano wao umekuepo toka lini?

Irene Uwoya: ‘Siku nyingi’
Soudy Brown: Msami kama namuona, unampa huduma zote?
Irene Uwoya: ‘Sanaaa kila kitu’
Soudy Brown: Uhusiano wenu utadumu au ndio kama wa Ndikumana?
Irene Uwoya: ‘Yakudumu kwa sababu nampenda’.
Soudy brown alimpa Irene taarifa kuwa mpenzi wa zamani wa Msami amekasirika kwa sababu Irene kaingilia mapenzi yao jibu kutoka kwa Irene likawa ‘hiyo haijalishi kwa sababu nampenda
Read more >>

PICHAZ TATA ZA IRENE UWOYA ZAZUA GUMZO MTANDAONI

Gal on fire she is back again staa irene uwoya, she was quite for a while, lakini ujio wake mpya alokuja nao umekuwa wa kishindo n people were so suprised, kiukweli kwa staa kibongo bongo nowdayz kuvaa taulo na kupiga picha akivaa taulo na kutupia kwenye mitandao ya kijamii ni jambo la kawaida sana.

Leo mtandaoni tumezinyaka picha hizi kwenye mitandao ya jamii, na fans wakawa wanacoment, kuna wengine walicoment kawaida wengine waliponda, but all in all kwa mastaa kama Irene Uwoya kuvaa taulo hauoni kama ni ki2 cha ajabu coz everybody do so. Alisikika akimalizia kisema hvyo kwa fans wake. 
Read more >>

IRENE UWOYA ANAHALI MBAYA, ALAZWA HOSPITAL YA AGHA KHAN

Irene Uwoya
Irene Uwoya katika pozi

Taarifa zilizosemwa na rafiki wa karibu wa msanii Irene Uwoya ni kuwa yupo katika hali mbaya zaidi na kufikia hatua ya kulazwa katika hospitali ya Agha Khan akisumbuliwa na Malaria.


Get well soon Irene....
Read more >>

UWOYA AJICHORA TATOO YA MIGUU YA MWANAYE MGONGONI.


Staa  wa muvi za Bongo, Irene Pancras Uwoya ameonesha upendo wake kwa mwanaye Krrish Ndikumana kwa kujichora ‘tatuu’ mgongoni yenye nyayo (makanyagio) ya mtoto huyo na kuzisindikiza na jina lake kwa juu.
Baada ya mchoro huo kukamilika, Uwoya aliitumbukiza kwenye mtandao wake wa kijamiii wa Facebook na kutazamwa na watu kibao ambao waliipenda.
Hata hivyo, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi  wetu kuhusiana na tatuu hiyo walisema Uwoya amefuata nyayo za wanawake wengi wa Kiafrika ambao wakishazaa huwapenda sana watoto kuliko baba zao.
 
“Picha ni nzuri, mama ameonesha upendo wake kwa mtoto lakini hii ni tabia ya wanawake wengi wa Kiafrika, wakishazaa mapenzi yote wanayahamishia kwa watoto badala ya waume zao.
 

“We fuatilia utagundua ndoa nyingi huanza kuyumba baada ya mke kujifungua, maana mapenzi yote yanahamia kwa mtoto, mume kama hana subira anaanza kutafuta mwanamke mwingine wa kumpenda upya.

“Inawezekana Uwoya mwilini mwake hana tatuu hata moja ya mumewe, lakini Krrish kamchora nyayo ili kuwaoneshea wadau wake,” alisema Oscar Samuel, mkazi wa Mwenge, Dar.
Read more >>

"NILIPOFUMANIWA DIAMOND NDIKUMANA WANGU ALIZIMIA"......UWOYA...!!

Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.

Ndikumana, alianguka na kuzimia, asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya, aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe, aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani ndiye aliyemsababishia majanga yote.
Hivi sasa, Ndiku yupo Rwanda, alitimka nchini baada ya kusoma habari ya Uwoya na Diamond kunaswa hotelini, ila kabla ya kuondoka, alitamka rasmi kuvunjika kwa ndoa yao.
Habari ya kuvunjika kwa ndoa, ilitoka kwa Uwoya mwenyewe ambaye alimweleza mwandishi wetu siku Ijumaa Wikienda, lilipodondosha ‘jiwe’ hilo mtaani. Uwoya alisema: “Na ndoa yenyewe imevunjika asubuhi ya leo, kila kitu kimeharibika.”
KWELI ANAJUTA KUMFAHAMU DIAMOND
Uzungumzaji na hata sauti, ni dhahiri Uwoya hataki tena kumsikia Diamond, kutokana na ukweli kuwa ‘brazameni’ huyo, amemharibia kila kitu, ikiwemo kuipeleka kaburini ndoa yao.
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Uwoya na mwandishi wetu;
MWANDISHI: Habari za kazi?
UWOYA: Salama tu.
MWANDISHI: Vipi shemeji yetu hajambo?
UWOYA: Shemeji gani? (anatukana) mume wangu ameniacha kisa stori ya Diamond.
MWANDISHI: Duh, imekuwaje tena jamani?
UWOYA: Alipoona stori ya mimi kuwa hotelini na Diamond, aliumia sana. Akaanguka na kuzimia.
MWANDISHI: Shida ilikuwa habari ya Diamond au mgogoro ndani ya ndoa?
UWOYA: Alipoona ile habari kwenye gazeti alianguka ghafla, akazimia kisha alipozinduka akarudi kwao. Ameamua kuniacha sijui kama atanirudia.
MWANDISHI: Pole sana, kwa hiyo familia yako inasemaje kuhusu hilo?
UWOYA: Familia yangu imenitenga kwa sasa.
MWANDISHI: Pole sana Uwoya.
UWOYA: Haina haja. Andikeni tu, mume wangu amenitosa rasmi.
MWANDISHI: Kwani amekupa talaka ndugu? Maana ndoa haiwezi kuharibika kirahisi.
UWOYA: Mimi na wewe hatutaniani, nakwambia ndoa yangu haipo tena.
MWANDISHI: Lakini shemeji yetu anakupenda sana.
UWOYA: Unataka kuandika hayo? Ukweli familia yangu haitaki kabisa kusikia habari za Diamond.
MWANDISHI: Kwani magazeti ya Global hayajasaidia kurejea kwa ndoa yako?
UWOYA: Mliandika habari nzuri ya ndoa yetu, tukarudiana, mlinisaidia sana na familia ilifurahi kuona hayo kwa wakati huo.
MWANDISHI: Sasa nani wa kulaumiwa juu ya ndoa yako?
UWOYA: Mimi niko ‘siriaz’, nimeachwa.
MWANDISHI: Ok, asante ndugu.
UWOYA: Asante, Mungu atawalipia tu.
KUHUSU DIAMOND NA UWOYA
Machi 25, mwaka huu, Diamond na Uwoya, walinaswa na kamera za Global Publishers Ltd (nyumba kubwa ya magazeti pendwa), kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Ijumaa Wikienda ambalo ni gazeti ndugu na hili, lilianika kila kitu, huku likiwa na ushahidi wa kutosha jinsi Diamond na Uwoya, walivyolala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, wakiingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
Read more >>

BAADA YA KUNASWA LIVE NA DIAMOND WAKILA URODA JOKETI 'KIDOTI' AMKEJELI IRENE UWOYA...!!

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ameangua kicheko baada ya kusikia mwigizaji Irene Uwoya kunaswa hotelini na Nasibu Abdul ‘Diamond’.


Jokate aliangua kicheko hicho juzikati jijini, Dar wakati alipozungumza na paparazi wetu na alipogusiwa kuhusu suala la Uwoya kunaswa na Diamond, alicheka sana huku akimshangaa.
“Hahaha sasa ndiyo nini tena, yeye si aliwahi kunisema mimi nakwapua mabwana? Sasa leo imetokea kwake tena!” alisema Jokate.
Read more >>

"UWOYA NI SIKIO LA KUFA"....MWAKIFAMBA




RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Saimon Mwakifwamba amefungukia ishu ya msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni mke wa mtu, Irene Uwoya kunaswa hotelini na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusema mdada huyo ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa.

Akizungumza kwa uchungu na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema Uwoya hajitambui wala hajiheshimu kwani ni siku chache tu alirudiana na mumewe Hamad Ndikumana lakini inashangaza kunaswa akiwa na Diamond hotelini.

“Uwoya anatakiwa kujitambua kuwa ana nafasi gani katika jamii pia kwenye ndoa yake kwani maisha anayoishi siyo mazuri na yanatia aibu familia na tasnia nzima ya filamu hivyo abadilike,” alisema Mwakifwamba.
Read more >>

BAADA YA KUNASWA NA UWOYA WAKILA URODA, DIAMOND SASA ASAMBARATISHA RASMI NDOA YA NDIKUMANA NA IRENE UWOYA, PENNY NAYE ATISHIA KUITOA MIMBA YAKE...!!

JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa.

http://4.bp.blogspot.com/-K3ZLArV45TM/Tsnm0_PownI/AAAAAAAAB8A/cjBwogrkXWw/s1600/19.jpgHabari ya wawili hao kunaswa na kubainika kulala katika chumba kimoja namba 208 kwenye hoteli maarufu iliyopo katika Ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi Beach jijini Dar, ilichapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, toleo namba 310 la Jumatatu ya Aprili 8-14, mwaka huu.
Mara baada ya habari hiyo iliyoshtua wengi kusambaa kama moto wa kifuu, watu mbalimbali waliliambia Amani kuwa hatimaye Diamond amemalizia kukata uzi wa mwisho wa ndoa ya Uwoya aliyofunga na msakata kabumbu, raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwaka 2009.

KAMERA ZETU
Vyanzo mbalimbali vilikiri kuwa ama kweli kamera zetu ni kiboko katika kutafuta ukweli wa jambo kwani ilikuwa ni minong’ono tu kuwa Diamond anatoka na Uwoya ambaye ni mke wa mtu japokuwa hakukuwa na ushahidi, lakini sasa mambo hadharani.
“Hata kama Ndiku (Hamad Ndikumana) alikuwa haamini sasa kila kitu kipo wazi, sidhani kama hapo kuna ndoa tena. Anataka ushahidi gani zaidi ya huo? Habari ya Ijumaa Wikienda imemaliza kila kitu,” alisema rafiki wa karibu wa Uwoya.

Habari zilieleza kuwa hata wasanii wenzao nao walishtushwa na habari hiyo iliyoweka rekodi kwa mwaka huu kwani kila mmoja alikuwa na lake la kusema huku wakimtupia lawama Diamond.
“Dah! Aisee ninyi  kiboko! Hivi huyu Diamond anaona raha gani kusambaratisha ndoa ya mwenzake? Alipotembea na akina Wema, Jokate, Wolper, Penny na Aunt Ezekiel haikuwa ishu sana kwa sababu hawakuwa kwenye ndoa. Lakini kwa Uwoya, amefanya kitu kibaya sana.
“Lakini hivi huyo dogo lengo lake ni nini? Au anataka kuwamaliza wote maana ameshapita nao sana na waliobaki ni wale ambao uzuri wao ni wa kumulika na tochi,” alisema staa mkubwa wa filamu wakati akisoma habari hiyo kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda.

NDIKU ATOWEKA
Habari za kina zilizonaswa na gazeti hili ni kwamba, mara baada ya kupata ukweli juu ya kusalitiwa na mkewe, Ndikumana ambaye alitua Bongo hivi karibuni alitoweka ghafla ikiwa ni siku chache tangu Uwoya alipotamba kurudiana naye na kuanza ukurasa mpya wa ndoa yao iliyokuwa mahututi.
Kupitia gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko toleo namba 996 la Jumatano ya Aprili 3-5, mwaka huu, Uwoya alitangaza kurejea kwa uhai wa ndoa yao huku wakioneshana mahaba kweupe.
Inaaminika kuwa ili kukwepa aibu hiyo baada ya kubumburuka kwa habari ya mkewe na Diamond, ndipo Ndiku aliyekuwa amejaa tele Bongo akatoweka na haijulikani alipo.
Wema Sepetu.
WEMA ANUNA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Wema, baada ya kusambaa kwa habari ya Uwoya kunaswa na Diamond, mwanadada huyo alinuna kwa kuwa wakati alipodai kuporwa mwanamuziki huyo na Jokate, Uwoya alikuwa mstari wa mbele kuponda kuwa jamaa huyo naye ni mwanaume gani huku akimwita Domo.
“Ukweli Wema amenuna maana hakuamini kama Uwoya anaweza kutembea na Diamond,” kilisema chanzo hicho.....
Read more >>

BAADA YA KUPATA SKENDO YA KUGAWA URODA KWA DIAMOND,IRENE UWOYA AAMUA KUELEZA YA MOYONI...!!


Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongomovies.com tuliamua kumtafuta kwa simu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kumuuliza juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi la mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” Diamond Platnumz.

Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari.

Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger