VAI WA UKWELI ASEMA TAMAA YA FEDHA ILINIPONZA, NAJUTA

SIKU chache baada ya msanii anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, ameibuka na kusema, anajuta, amekoma na hatarudia tena.
Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika ofisi za GPL akiongea na OFM.
Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita, ambapo msanii huyo aliingia mkenge baada ya kukubali kukutana na ‘pedeshee’ mmoja kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda kwa malipo ya shilingi 500,000.
Vai alivyonaswa akiwa mawindoni.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, Jumatatu jijini Dar es Salaam, Vai alisema: “Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba ndugu zangu na mashabiki wangu wote wanisamehe kwa dhati kabisa.
Vai akificha sura yake baada ya kunaswa na OFM.
“Naahidi sitarudia tena ujinga kama ule. Ilikuwa ni tamaa tu. Hivi ninavyozungumza na wewe nipo kwa editor (mhariri) nasimamia editing (uhariri) ya filamu yangu ambayo ipo katika hatua za mwisho kuingia mitaani. Niko bize na kazi, acha niwekeze kwenye ujasiriamali tu. Nawashauri wasanii wenzangu tutulie maana OFM wapo macho.”
...Akimsubiri pedeshee.
Alisema, katika filamu yake hiyo aliyoipa jina la Beautiful Liar amewashirikisha wakongwe Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Hashim Kambi ‘Wingo’ na mastaa wengine kwenye tasnia hiyo na kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kula.
...Baada ya mchezo kuharibika.
Kuomba msamaha ni uungwana, ikiwa Vai umeona kosa lako na kuomba radhi ni jambo zuri la kupongezwa. Tunakutakia kila la heri katika mabadiliko hayo, tukikusisitiza iwe kweli maana OFM bado ipo kazini. – MHARIRI.
Read more >>

NJEMBA YABAMBWA IKIIBA KANISANI, AGEUZWA BUCHA!

KIOJA! Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo ‘hevi’ baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
Wanachuo wakikagua baadhi ya vitu alivyokutwa navyo Emmanuel.
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.
Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo wenye hasira.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali huku wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Emmanuel akiwa na vitu vya wizi alivyokutwa navyo.
Kama kawaida, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona jamaa huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.

Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama  ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.
Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.

Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa hasira.
Read more >>

MBONGO ALIYEBAKWA HADI KUFA CHINA... MAMBO MAKUBWA YAIBUKA!

KATIKA Gazeti la Ijumaa Wikienda la juzi Jumatatu, Toleo Namba 354 ukurasa wake wa mbele kuna habari yenye kichwa kisemacho; MBONGO ABAKWA CHINA, AFA!

Sabrina enzi za uhai wake.
Katika habari hiyo, kulisindikizwa na vichwa vidogo vilivyosomeka; Wabakaji ni Wanigeria watano, maiti yake yakutwa haina figo, moyo!
Habari hiyo ilimhusu Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Sabrina au Habiba kwamba, aliondoka Bongo kwenda Guangzhou, China akidanganywa na mwanamke mmoja kwamba anakwenda kufanya kazi kwenye saluni ya kike.

Habari zilisema baada ya kufika China, mwanamke huyo alimnyang’anya Habiba hati ya kusafiria na kumwingiza kwenye biashara ya ukahaba kwa kumuuza kwa wanaume huku ujira akiuchukua yeye.
Ilidaiwa kuwa, tabia hiyo ndiyo iliyopo kwa sasa kwamba, kuna wasichana wanachukuliwa kupelekwa nchini humo kwa kudanganywa kufanya kazi saluni matokeo yake huishia kwenye ukahaba.

NDUGU WASOMA GAZETI, WAJITOKEZA
Sasa, baada ya gazeti hilo kuingia mtaani siku hiyo, mazito yakaibuka.
Ndugu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa marehemu alimpigia simu Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka na kumweleza kuwa wamesoma habari za kifo cha Habiba kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Akizungumza kwa sauti iliyojaa simanzi, ndugu huyo alisema nyumbani kwao ni Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.
Mhariri: Ndugu poleni sana! Je, naweza kutuma waandishi wangu wakafika hapo na kujua mawili matatu kuhusu marehemu?

Ndugu: Hamna tatizo, baba yupo ila mama alikuwa Vikindu (Dar) ndiyo anakuja yuko njiani.
Mhariri alituma waandishi wawili kufuatilia mkasa huo ambao umewatikisa Wabongo waishio eneo la Guangzhou nchini China.

WAANDISHI MSIBANI, WAKUTANA NA BABA MZAZI
Akizungumza msibani, baba mzazi wa marehemu, mzee Yusuf Ally alisema Habiba  aliondoka nchini kwa kutoroka kwenye Sikukuu ya Idd El Haj mwaka 2012.

Alisema hakuwa na mawasiliano mazuri na bintiye huyo si kwa sababu ya kutoroka tu bali kwa vitendo alivyokuwa akivifanya na kila alipomuonya binti huyo hakusikia, mwishowe akaamua kukata mawasiliano naye.
“Sikuwa na mawasiliano na Habiba tangu Machi 2010 kwani aliniudhi sana,” alisema mzee huyo licha ya kwamba alikuwa akiporomosha machozi kufuatia taarifa za kifo cha binti yake.
NINI HASA UGOMVI WA HABIBA NA BABA YAKE?
Akiendelea kusimulia maisha aliyokuwa akiishi na mwanaye huyo, mzee Yusuf alisema:
“Habiba alibadilika tabia akawa hataki kusoma. Mbaya zaidi kilichonikera ni pale alipokataa kwenda kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2010. Kiukweli iliniuma sana.

“Nilimsomesha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, nilikuwa najinyima kula kwa ajili yake, siku ya mtihani akakataa kwenda shule, niliumia sana hasa nikikumbuka fedha zangu nilizotupa kwa ajili yake,” alisema.
JINSI ALIVYOONDOKA BONGO
Naye dada wa Habiba, Aziza Said ambaye alikuwa akiishi na marehemu alisema kwamba ilikuwa siku ya Idd El Haj mwaka 2012 ndiyo siku ambayo mdogo wake huyo alitoroka nyumbani na kwenda kujificha kusikojulikana.

“Siku hiyo nilimwachia fedha ili aende saluni akamsuke mtoto, mi nikaenda Kariakoo. Niliporudi nikakuta fedha za kusukia ziko mezani na mtoto anacheza nje.
“Nilimuuliza mwanangu mama mdogo yuko wapi? Akanijibu hajui. Sikuwa na wasiwasi kwani nilijua alikwenda kwa mashoga zake kula sikukuu, kwangu alihisi ningembana. Kumbe mwenzangu yuko katika mipango  ya kutoroshwa nchini,” alisema dada huyo na kuangua kilio.
MWANAMKE ALIYEMTOROSHA WANAMJUA
Familia hiyo ilisema mwanamke aliyemtorosha Habiba kutoka Bongo kwenda China wanamjua (jina tunalo) kwani waliwahi kuishi naye nyumba moja, Manzese jijini Dar lakini wakawa hawaongei naye kwa sababu ya tabia zake mbaya.

Walisema mwanamke huyo alianza kumbadili tabia Habiba miezi michache kabla ya safari ya China, hasa kwa mavazi ya ajabu na tabia ya kutotulia nyumbani.
Waliendelea kusema kuwa, ilifika mahali kutokana na tabia yake mpya isiyo na maadili, waliamini binti huyo ametumbukia kwenye mambo ya kigodoro (ngoma za uswahilini).
MARA YA MWISHO KUONEKANA WHATSAPP
Kaka wa marehemu Mohammed Yusuf Ally  alipoongea na gazeti hili msibani hapo alisema kuwa mara ya mwisho kufanya mawasiliano na marehemu ilikuwa Valentine’s Day (Sikukuu ya Wapendanao)  – Februari 14, mwaka huu, ambapo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno katika Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp lakini meseji hiyo  haikujibiwa.

“Nimeshtuka sana leo kupata taarifa kwamba mdogo wangu amefariki dunia tena baada ya kusoma gazeti (Ijumaa Wikienda) huku kifo chake kikiwa cha kikatili kiasi hicho,” alisema akilia kaka huyo.
NYONGEZA NYINGINE YA TAARIFA
Kwa mujibu wa ndugu, mbali na miongoni mwao kulisoma Gazeti la Ijumaa Wikienda na kupata taarifa, lakini kwa mzee Yusuf habari zilimfikia baada ya jirani kununua gazeti hilo na kumpelekea nyumbani hapo.

KAKA AISHUKURU GLOBAL
“Nalishukuru hili gazeti (Wikienda) kwani bila ya wao kuandika tusingejua nini kinaendelea huko China,” alisema kaka wa marehemu huku akiwa ameshika gazeti hilo.
Read more >>

HIVI NDIO JINSI USTADH KICHAA ALIVYOMCHINJA MTOTO

KUFUATIA tukio la Ustadh Mohamed Said Ngulangwa (36), mkazi wa Mbagala-Charambe jijini Dar kumchinja mtoto Jamal Salum Ally (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano kisha na yeye kuuawa na wananchi wenye hasira, Uwazi kama kawaida yake lilichimba tukio hilo na kubaini mengi, twende pamoja.
Mtoto Jamal Salum Ally (12) enzi za uhai wake.
MTOTO AITWA, AENDA
Akizungumza na Uwazi Jumamosi iliyopita msibani Mbagala juzi, mtoto mmoja (jina lipo) alisema yeye na marehemu walikuwa wakicheza michezo ya kawaida, mara akatokea ustadh na kumwita mtoto Jamal.

Ustadh Mohamed Said Ngulangwa (36) enzi za uhai wake.
“Sisi tulikuwa tunacheza, ghafla ustadh akamwita Jamal. We Jamal, njoo. Kwa vile aliita kwa sauti ya kawaida tulijua anataka kumtuma, Jamal akaenda mimi nikawa namsubiria ili tuendelee kucheza, kumbe mwenzangu aliitwa kuchinjwa,” alisema mtoto huyo kwa sura iliyojaa simanzi.
Waombolezaji wakiwa msibani.
KISU KIKALI CHATUMIKA
Mtoto huyo aliendelea kueleza kwa uchungu kwamba, akiwa anamshuhudia Jamal akikutana na ustadh, alishangaa kumwona mwanaume huyo akimdaka kwa haraka na kisha kutoa kisu ambapo alianza kumchomachoma nacho na hatimaye kumlaza chini na kukipitisha shingoni kama anachinja kuku.

Mwili wa ustadh baada ya kuuawa na wananchi wenye hasira kali.
“Nilipiga kelele kuwaambia watu, nikatoka kwenda kuwaita watu huku napiga kelele kwamba Jamal anachinjwa na ustadh,” alisema mtoto huyo huku akionesha sura halisi ya masikitiko ya ndani ya moyo. Inauma sana!
Mwili wa mtoto Jamal baada ya kuchinjwa na ustadh.
MAJIRANI WADHANI ADHABU INATOLEWA
Nao majirani na madrasa ya mtu huyo waliopata nafasi ya kueleza walichojua kuhusu mauaji ya mtoto huyo, walisema kelele za mtoto Jamal kuomba msaada zilisikika, lakini waliamini mtoto anapewa adhabu na mzazi wake.

MAMA WA MAREHEMU AFIKA MBIO
Maelezo zaidi yanasema kuwa, mtoto aliyekwenda kuita watu alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu na kumkuta mama mzazi ambaye alimpa taarifa.

Eneo alilochinjiwa mtoto Jamal.
Mwanamke huyo aliyepewa taarifa hizo, akiwa haamini masikio yake, alitoka mbio na kilio kuelekea eneo la tukio.
Wananchi nao baada ya kusikia maelezo ya mtoto aliyeshuhudia, waligutuka na kutua eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikutana na kichwa kikiwa miguuni mwa kiwiliwili. Lazima umwage machozi!
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
MBALI NA KIWILIWILI NA KICHWA
Wananchi hao waliweza kugundua kuwa, kichwa hicho ni cha mtoto Jamal huku pembeni yake kukiwa na ndoo ambayo walidai muuaji alikusudia kukingia damu (ili iweje?).

VILIO VYATAWALA, USTADH AJIFICHA
Vilio vilianza kutalawa eneo hilo, akina mama, marafiki wa marehemu waliangua vilio vya uchungu baada ya kuuona ukatili huo ambao walisema haujawahi kutokea katika eneo hilo.

Jeneza lenye mwili wa Jamal likiwa mbele ya waombolezaji.
Ilidaiwa kwamba, wakati huo ustadh alikuwa amejificha chumbani kwake ili kuepuka ‘soo’ lake lakini wananchi walishtukia janja yake na kutishia kuvunja dirisha ambapo mtuhumiwa huyo alichungulia akiwa na kisu mkononi kikiwa na mabaki ya damudamu.
WANANCHI WAVUNJA MLANGO, DIRISHA LA USTADH
Bila kujali kisu hicho, wananchi walivunja mlango na dirisha na kuanza kumshambulia kwa mawe, kisha wakamchomoa akiwa uchi wa mnyama mpaka nje huku wakiendelea kumshambulia hadi akakata roho.

Magari ya polisi yakiwa eneo la tukio.
BABA WA MAREHEMU NAYE ANALO NENO LA KUSIKITISHA
Naye baba wa Jamal, Salum Ally alipoongea na Uwazi alitoa simulizi ya majonzi, msikie: “Nilipokea kifo cha mwanangu Jamal kwa huzuni kubwa sana, sikuamini kama yeye ndiye aliyeuawa kikatili namna ile!

“Nilikuwa narudi nyumbani kutoka kazini, jirani na nyumbani nikakuta watu wengi, nikahoji kulikoni? Nikaambiwa kuna mtoto amechinjwa na aliyemchinja ameuawa. Khaa! Nikashangaa!
Baadhi ya watoto waliofika eneo la tukio kushuhudia mwenzao aliyechinjwa.
“Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana, niliona nifike kwangu kwanza ndipo nirudi kwenye tukio. Kabla ya kutua kwangu, nikakutana na mke wangu njiani huku akilia, nilipomhoji kuna nini, aliendelea kulia bila kunipa majibu.
“Ndipo mpangaji mwenzangu akanipasulia kwa kuniambia kwamba mwanangu Jamal amechinjwa mpaka kichwa kutenganishwa na kiwiliwili.
“Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani sikufikiria kama kungetokea tukio la kutisha kama hilo, hata kama mngekuwa ninyi waandishi mngefanyaje jamani?
Mwili wa Jamal ukiombewa kabla ya maziko.
“Nilijivuta hadi eneo la tukio na kukuta mwili wa mwanangu umeshafungwa kwenye nguo na kuwekwa ndani ya gari la polisi, sikuwa na nguvu ya kuangalia sura yake kwa uchungu nilioupata kwani ndiyo mtoto wa kwanza,” alisema Salum.
USTADAH ALIPANGA MAUAJI?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, ustadh huyo alijiandaa kutekeleza mauaji hayo kwa vile aliandaa kisu na ndoo kwa ajili ya kukingia damu ya mtoto huyo kwa kile watu walichodai alitaka kuinywa.

POLISI MZIGONI
Baadaye taarifa zilienea maeneo yote ya Jiji la Dar hususan Mbagala-Charambe na polisi walitua eneo hilo na kuchukua miili ya marehemu wote wawili na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Temeke.

Mwili wa Jamal ukipelekwa eneo la makaburini kwa maziko.
Pale hospitalini, madaktari walitumia saa mbili kichwa cha mtoto Jamal na kiwiliwili.
USTADH ATAJWA KUTOKUWA NA AKILI
Mdogo wa Ustadh Mohamed aliyekuwa msemaji wa familia, Daudi Ngulangwa alisema marehemu kaka yake aliwahi kupatwa na ugonjwa wa akili mwaka 1995/96 kisha kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutibiwa na akapona.

Maziko ya mtoto Jamal yakifanyika.
MAZISHI YAO
Marehemu Jamal alizikwa Jumamosi iliyopita katika Makaburi ya Mbagala-Charambe jijini Dar (Uwazi lilikuwepo).
Ustadh Mohamed, yeye alizikwa siku hiyohiyo kwenye Makaburi ya Manzese jijini Dar es Salaam.
Read more >>

MASOGANGE NI BORA UKATE MAONO KAMA HIVI KULIKO KUUZA SEMBE

Week hii Mitandaoni zimetawala picha za Agness Masogange Mitandaoni Akicheza jukwaani huku akionehsa kiuno chake kwa chati kwenye ufunguzi wa Pub Moja huko Dodoma Its Obvious Alilipwa kwa kufanya hivyo tena si hela ndogo ...Mimi ki  ukweli kanifurahisha ni bora atumie kipaji chake na umbo lake kujipatia hela kwenye matamasha ama video mbali mbali kuliko ile ya kuuza Sembe aka Ungaz....Hongera Masogange......Au unasemaje mdau ?
Read more >>

SINTAH "NASHUKURU LE MUTUZ UMENISIKILIZA..ACHANA NA VINUKA MKOJO"

"Nashukuru umenisikiliza my ndugu Le Big show Le Mutuz nilikwambia na kila siku nikiongea na wewe nakwambia, achana na vinuka mkojo wa mitaani , unakaa na watu wasiongea mambo ya maana  kuanzia asubuhi wakiongea la maana ni ku snitch mtu, wewe ongea na matajiri wakuambukize harufu nzuri ya ankara sasa nakuona jinsi unavyo shine, mie tangu nijue hiyo kanuni sipati shida na mtu nni mwendo wa salamu, unacheka nao wabaya ni haohao, usnitch umetawala kila sehemu kazini, majumbani, kwenye familia seriously u dont know who to trust , ila umeniuzi mbona hukunichukua kwa Ken na mie nikatoe maada zangu si unajua beauty plus brain, usingekuwa disappointed, next trip usiniache....

Big up na endelea kunisikiliza utapata mengi ......"SINTAH
Read more >>

EMBU JIONEE MWENYWE HUYU ALIVYOPIGWA NA BOYFRIEND WAKE



Her name is Gabriella. Says she's an aspiring Victoria Secret model and actress. Not sure where she's from though. Gabriella, via her instagram account @bambiiiii_ shared her recent sad experience of domestic violence from her boyfriend of eight months. She was badly beaten, thrown from a moving vehicle and dragged. She shared this photo of her injury above on her instagram page and wrote:
"This might be a little graphic but I just want to let everyone know that I am okay. I am a survivor of domestic violence with a boy I dated for 8 months. I really thought everything was fine but he constantly questioned me about cheating and flirting. Nonsense. I never looked at someone the way he looked at me. Thought I loved this boy. How can someone that 'loves' me do this to me? The scars on my chest are way worse and extend down to my right nipple, completely scarred. The skin on my shoulder has been completely skinned. And I have bruising on my rib cage, neck, and my muscles. I was kicked out of a moving vehicle, then beaten and dragged, as I blacked out and was left lying there in my own puddle of blood. Doctors said I could have died if not made it when I did. I am so blessed and beyond lucky to be alive and have so much support from friends, family, and strangers. As I try to recover I ask to please keep me in your prayers. I have to wear a neck brace for 3-4 weeks, an arm cast and I can barely walk for now. Thank you for all the love. I hope to be an inspiration to women and anyone involved in domestic violence.
She didn't say what happened to the guy that did this. See pics of Gabby before the brutal attack after the cut ...

Read more >>

MAJANGA:MAJANGA:MAJANGA:MAJANGA:MAJANGAMAJANGA:MAJANGA

Photo: Mtu huyu alipata ajali akiwa anaelekea kazini asubuhi moja.

Kutokana na ripoti walizotoa majirani na wana familia ni kwamba aliondoka nyumbani akiwa amechukia na kuhuzunika kwa kuwa hana hela ya kulipia pango na pia mama yake ni mgonjwa na anahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu.......Jambo lililomfanya akatishwe tamaa na kuwa na msongamano wa mawazo

Akiwa katika dimbwi la mawazo akajisahau kuangalia upande wa pili mpaka lori likamgonga na kumvunja mguu.

Ni binadamu kama mimi na wewe, hebu angalia yaliyomkuta kwa sababu ya mawazo ambayo wote tunayo katika maisha yetu ya kila siku.

Mungu atunusuru na kutupa mioyo ya uvumilivu na tuyahimili matatizo yanayotukabili sisi na familia zetu na yasituletee mamatizo na ya kutuharibu kabisa.

Mungu amponye na kumpa nafuu ya maisha huyu ndugu.

•Tafadhali usipite bila kuandika neno AMEN...
Mtu huyu alipata ajali akiwa anaelekea kazini asubuhi moja.
Kutokana na ripoti walizotoa majirani na wana familia ni kwamba aliondoka nyumbani akiwa amechukia na kuhuzunika kwa kuwa hana hela ya kulipia pango na pia mama yake ni mgonjwa na anahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu.......Jambo lililomfanya akatishwe tamaa na kuwa na msongamano wa mawazo
Akiwa katika dimbwi la mawazo akajisahau kuangalia upande wa pili mpaka lori likamgonga na kumvunja mguu.
Ni binadamu kama mimi na wewe, hebu angalia yaliyomkuta kwa sababu ya mawazo ambayo wote tunayo katika maisha yetu ya kila siku.
Mungu atunusuru na kutupa mioyo ya uvumilivu na tuyahimili matatizo yanayotukabili sisi na familia zetu na yasituletee mamatizo na ya kutuharibu kabisa.
Mungu amponye na kumpa nafuu ya maisha huyu ndugu.
 Tafadhali usipite bila kuandika neno AMEN, KWENYE PAGE HII https://www.facebook.com/pages/BONGO/475899065866363
PIA USISAHAU KULIKE PAGE HII
Read more >>

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMETOKA, YATAZAME HAPA KIURAHISI

Matokeo ya kidato cha nne sasa yametoka rasmi hewani, kuwa wa mwanzo kuyaona kwa njia rahisi zaidi, Pia usisahau kulike page yetu ili uwe unapata habari zetu kirahisi zaidi
bofya hapa kuyaona<<https://www.facebook.com/pages/BONGO/475899065866363>>
Read more >>

WALE WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA WARUDI NCHINI BAADA YA KUTENGANISHWA NCHINI INDIA



  Watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha wakiwasili nchini Tanzania kutokea nchini India walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya watoto ya Appolo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe, mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph.


 Watoto hao wakiwa wamebebwa na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph (kushoto) na mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel.



Mama  mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel akiwa amewabeba watoto wake Elikana Erick (kushoto) ns Eliud Erick (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.



 Habari na picha na 

Aron Msigwa – MAELEZO.

Hatimaye watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha jana jioni wamerejea nchini wakitokea nchini India katika hospitali ya watoto ya Appolo walikokuwa wanapatiwa matibabu.
 
Mara baada ya kuwasili katika  Uwanja ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakiwa wameambatana  na mama yao mzazi Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph wamepokewa na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe  na baadhi ya wauguzi kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) .
 
Mapacha hao wa kiume wakiwa wenye  furaha na afya njema walichukuliwa katika gari maalum na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambako watakaa kwa muda mfupi na kisha kuruhusiwa kuelekea wilayani Kyela jijini Mbeya ambako ndiko walikozaliwa.
 
 Kwa upande wake mama mzazi wa watoto hao akizungumza kwa furaha mara baada ya watoto wake kupatiwa matibabu ya kuwatenganisha kwa mafanikio makubwa amesema kuwa sasa maisha yake yamebadilika na ataishi kwa furaha na watoto wake.
“Najisikia furaha sana kwa hatua niliyofikia mpaka hapa watoto wangu Eliudi na Elikana sasa ni wazima naishukuru sana Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa msaada ilionipatia” amesema.
 
Kwa uipande wake Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph akizungumzia matibabu ya watoto hao nchini India amesema kuwa hatua ya kuwatenganisha imekamilika na mwezi wa 8 mwaka huu watarudi tena nchini India kwa  ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi ya afya zao.
 
“Ni kwamba watoto hao wametenganishwa, kwa wakati huu wanaelekea MOI ambako watakaa kwa muda na baadaye wataruhusiwa kwenda kwao Mbeya kujumuika na jamaa zao” amesema.
 
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja amesema kuwa watoto hao waliwasili jana jioni na ndege ya shirika la ndege la Oman baada ya kumaliza matibabu ya awamu ya kwanza.
 
Amesema upasuaji huo mkubwa wa kuwatenganisha watoto hao ulichukua saa 18 na kufafanua  kuwa kati ya hizo  saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo,sehemu ya utumbo mpana,njia ya mkojo,kibofu cha mkojo na sehemu za uume huku saa 5 zikitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.
 
“Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mpaka sasa duniani upasuaji wa aina hii umefanikiwa mara tano  kutenganisha mapacha watoto wa kiume walioungana” amesisitiza.
 
Ameongeza kuwa matibabu hayo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa  kwa kila mwananchi kila inapowezekana na kutoa wito kwa jamii kujenga utaratibu wa kuwafikisha mapema kwenye vituo vya afya wale wote wenye matatizo ya kiafya badala ya kuwafikisha pindi hali zao zinapokuwa mbaya.
Read more >>

MWENYEKITI WA CHAMA CHA NLD ALIJITEUA YEYE NA MKEWE KWENYE BUNGE LA KATIBA, WADAU WALALAMIKA


Habari kwa mujibu wa gazeti la MWANANCHI — Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.

Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, 2013 kwa kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.

Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa.

Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar... 

“Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake nikapeleka majina manne, tukapata uwakilishi.”
Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa zake... 

“Wanalalamika nini hata chama tawala cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mkewe Salma pia ni mjumbe wa NEC.”
Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.

Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.
Read more >>

MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA AUNDA TUME YA WATU 6 ITAKAYOTAZAMA JINSI YA KUONGEZA POSHO SH. 300,000 KWA SIKU


Suala la posho limezidi kuwa kaa la moto katika vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma leo, hali iliyomlazimu mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho ateue timu maalum ya watu 6 kutazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo. 
 
Timu hiyo inatarajiwa kuyachunguza kwa undani mahitaji ya wajumbe wa Katiba, kisha kuisaidia serikali kutafuta jinsi ya kuongeza posho hizo.
 
Wajumbe wa timu ya posho ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
 
Wengine ni mjumbe wa asasi zisizo za kiserikali Paul Kimiti, Mbunge wa Peramiho Jenister Mhagama (CCM) na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Asha Bakari na Mohamed Aboud Mohamed.
 
Huku hayo yakiendelea Dodoma, Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa amedai  kuwa posho wanayopewa wajumbe ya Sh 300,000 kwa siku inatosha kabisa, “kwa kuwa hata wafanyakazi wengine wa serikali wanapokea mshahara wa laki tatu mwisho wa mwezi.”
 
Mwenyekiti Msaidizi wa CUF, Julius Mtatiro anaunga mkono mtazamo huu. Katika waraka wa wazi aliouweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mtatiro anaandika:
 
“Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha kabisa, ambaye hazimtoshi aongeze za kwake [ama] aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa posho ya Sh 300,000 waendelee.”
Read more >>

MCHUNGAJU MTIKILA ASEMA BUNGE LA KATIBA LIMEJAA WAHUNI NA

Mchungaji Mtikila leo huyu jamaa amekandia bunge lote la katiba na kusema anasikitka soon ataliacha bunge hilo mana limechaguliwa kihuni.
Nasema hivi wambieni kabsa nimesema hili ni bunge la kihuni limechaguliwa kihuni ndio maana unakutana na mambo ya kishenzi mnayoendelea kuyaona.

Nasema tangia uhuru sijapata kuona bunge la kihuni kama hili.

Sitoshangaa maamuzi ya kihuni na
kishenzi kutokea siku tunaagana pale nje.
Huyo ni rev. Christopher Mtikila.

Source: BBC swahil
Read more >>

FACEBOOK SASA KWAINUNUA WHATS APP



San Fransisco. Mtandao wa kijamii wa Facebook umenunua programu ya huduma za meseji ya WhatsApp kwa dola za marekani bilioni 19 (TSh 30.9 trilioni) katika taarifa iliyotoka mapema leo.
Ununuzi huo wa WhatsApp umetengeneza mabilionea wapya angalau watatu, akiwemo mwanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum, ambaye atajiunga na bodi ya wakurugenzi ya Facebook.
Mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Brian Acton, naye anaingia katika orodha ya

mabilionea wapya vijana.
Miaka 4 iliyopita, Acton alijaribu kuomba kazi Facebook na Twitter baada ya kupunguzwa kutoka Yahoo, inaripoti blogu ya teknolojia ya Techcrunch.
Hakufanikiwa.
Leo hii, program aliyoitengeneza na rafikiye wa Yahoo, Koum, inagombaniwa na kampuni zilezile zilizomkataa na hatimaye, imenunuliwa kwa mabilioni ya dola na Facebook.
Wengine walioula ni wawekezaji wa kwanza wa WhatsApp toka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia.
Techcruch inaripoti vijana wa Sequoia wametengeneza zaidi ya dola bilioni 3 (TSh 4.9 trilioni) – mara 50 ya pesa waliowekeza – katika ‘dili’ hilo.
Facebook, ambao ni mtandao mkubwa kuliko yote duniani ukiwa na wanachama zaidi ya bilioni 1, inaamini kuwa WhatsApp itasaidia kuongeza uwepo wake katika masoko mbalimbali duniani, hasa katika nchi zinazoendelea Afrika, Asia na Amerika Kusini ambapo teknolojia ya simu za mkononi imeshika hatamu.
Uamuzi huo unaipa Facebook nafasi ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake, itarithi zaidi ya watumiaji milioni 450 wa WhatsApp.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg anaamini uamuzi wa kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19 ni wa busara, kwa kuwa “[WhatsApp] ni mtandao unaokuwa kwa haraka, ambayo itafikia watumiaji zaidi ya bilioni moja hivi punde.”
Read more >>

LINEX ACHANWA NA MAMA YAKE BAADA YA KUVISHA PETE MZUNGU

Sunday Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ kumvisha pete ya uchumba demu wake mtasha, Suvi Rikka, mama wa staa huyo, Imelda Barnabas ameibuka na kumchana mwanaye kuwa haitambui pete wala mchumba huyo kwa kuwa kitendo hicho hakina baraka zake wala za familia.

Shemeji yetu katika pose

Linex alipoulizwa juu ya sakata hilo, alifunguka:
“Yah! Bi mkubwa amenijia juu ile mbaya, ila najitahidi kumuomba msamaha, hope atanielewa.”
Read more >>

FUMANIZI:MKE AFUMWA AKIZINI NA SHEMEJI YAKE

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akingonoka’ na shemeji yake.
 
Tukio hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka mtego bali ni Mungu tu.
Alieleza kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa ‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.

“Jumapili jioni walikuja tena kuniletea chakula ila kwa bahati nzuri Jumatatu nikapewa onyo na kuachiwa. Cha ajabu nilipofika nyumbani nilimkuta mtoto wangu wa miaka 2 analelewa na majirani.

“Nilipowauliza mke wangu yuko wapi walidai tangu Jumamosi hajaonekana kwa maelezo kwamba amekwenda kushughulikia dhamana yangu,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa aliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali hadi alipoamua kwenda nyumbani kwa mdogo wake.
 
“Nilipofika nilimkuta mke na mdogo wangu wakiwa pamoja kitandani. Baada ya mdogo wangu kuniona alinyanyuka na kuvaa bukta kisha akatoka nduki,” alisema Mrisho. 
Ikaelezwa kuwa, baada ya mwanaume huyo kumfumania mkewe huku majirani wakishuhudia, alimshushia kipigo kisha akampa talaka kabla ya kuamua kumrudisha kwao Tabora.

Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na kufumaniwa huko, Bahati alisema shemeji yake alimlazimisha kulala naye baada ya kutoka polisi kumpelekea chakula mumewe.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Rehema Dimoso alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake
Read more >>

DAVIDO AFUNGUKA KUHUSU KASHFA ZINAZOMUANDAMA, SOMA HAPA



Baada ya skendo nyingi kumuandama msanii Davido kutoka Nigeria zinazohusiana na wanawake, mwenyewe aamua kufunguka na kuweka wazi kwa kila mtu. tazama hapo chini alichokiandika




Read more >>

WANAOWAREMBESHA KUCHA WANAWAKE, NDIO WANAOONGOZA KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU


Kama wewe ni mwanaume, huenda si wa kwanza kujiuliza maswali kila uonapo wanawake wengi wakiwa wamejipanga mstari kusafishwa kucha, kupakwa rangi kucha na kuoshwa miguu na vijana mbalimbali walioamua kujiajiri wenyewe. 
  


Ni biashara maarufu mjini na ambayo inazidi kukua kila kukicha. Katika biashara hiyo wanawake husafishwa kucha na kuoshwa miguu na wakati mwingine hadi sehemu za mwili za wanawake zinazokaribia maeneo ya mapaja (sehemu sensitive haswaa). Je! Shughuli hii ina madhara katika mahusiano? Vijana hawa wanaaminika?
nails-pedicure
Hiyo ni kwasababu kwa mujibu wa gazeti la Ijumaa imebainika kuwa baadhi ya wake wa vigogo na wanawake wengine nchini hufanya ngono na vijana hao wasafisha kucha na watengeneza miguu! Swali kwa wanaume: 
Unamruhusu mkeo/ mpenzi wako kwenda kupata huduma hii? Swali kwa wanawake: Kuna kitu gani special kwenda kusafishwa miguu badala ya kujisafisha mwenyewe nyumbani? Bongo5 wamekaribisha mjadala huu kwenye ukurasa  wa Facebook, na hivi ndivyo wadau wanavyojadili:
Brenda Hance: Ila jaman kupakwa rangi nao yes not bad koz wanapaka vizuri na kuturemba just like salun ila hyo ya kusuguliwa miguu sijui nn duuuh.
Mark Rose Msemwa: Kusafisha miguu na mikono ni taaluma kama taaluma nyingine, mengine ni hulka ya mtu. Mtengeneza kucha be professional, mwanamke be a good client.
Adams Davids: Nishawah mwona mwanamke eti anasafishwa miguu wakati nusu ya mwili wake uko mtupu afu kajiachia tu, na ndo maana wanauchezea afu walivyo na akili fupi wanapangwa tu kutokana na tamaa zao.
Haji Mushy: Ebwana wakina dada zetu wana tamaa sana cjui wapenz au waume zao huwa hawawaridhishi? Coz nshashuhudia matukio mengi dhidi ya hawa wapaka rangi na pia dada zetu wanavaa vimini wakati wanapokuja pakwa rangi…watu wazima na heshima zao mnaacha wanaume wenye hadhi!lllooo. Mpaka rangi mmmoja alimpa dem mmoja hv mimba iliyompelekea kuachana na masomo nakusota kitaa!til 2day!!! alikua chuo mwaka wa kwanza! Afu wengi wawapaka rang niwagosi mpaka leo ndug zake wamechukia wagosi.
Fredy Chackes: Sio kama kuna issue yyte ambayo ni xtra ordnary kwenye kusafisha kucha we hujajiuliza kwann wake wa vgogo kwa sana? ni hivi vgogo wengi wako busy na watoto wa dogo wa shule na vyuo, issue inakuja sasa wake zao pia ni binadamu wanakidh vp mahtaj ya mwili ndo jbu linaptkana kwa wasafisha kucha na vjana wengine pia simple tu.
Mohamed Mputi: Sioni ajabu hao vigogo mbona wapo bizz acheni wasaidiwe utakuta jamaa anakaa hata wiki mbili kila siku yeye anarudi usku kwanini mkeo asijisikie hamu ndoo maana hao vijana wanapomshika mkeo miguu tuu mwana mke anaanza kuhiss vibaya mara utasikia unanigusa vibaya alazima atamuliza tuu hapo ndoo shuhuli inanza mm naona nyee vigogo badilkeni wanawake nao watabadilika.
Bahati Nelly: Hahahaaaa,mbona wanaume wanaenda kufanyiwa massage,wanasuguliwa pia huko wanakandwa,mara pedicure,afu wanawachkua wadada wa humo,mkuki kwa nguruwe heheheee.

Ericka William: 
Hakuna lolote na wanaume wanavoenda kunyoa na kufanyiwa Scrub hko masaloon wao ndiyo sahiHi au kwann asimwambie mkewe amsugue? Maana mwanaume anasuguliwa uso na vidole vinapitishwa maskioni mpka anansinzia kha! Na kumtaka mtu ni hulka ya mtu tu na c kwenda kutengenezwa kucha saloon hakuhusiani kabisaa.

Emmanuel Mchicha: Hzo ni story2, kama dem wako unamfanyiaga u2ndu mwing kitandan mpaka anaridhka hawez kukusalit kwa msugua miguu.

Nasiri N Mussa: 
Wanawake ni watu wa kushawishka so anaweza akawa hajafkiria kufanya mapenzi lakini katka hali ya kushkwashkwa miguu anajikuta akimvumtia hisia mtu anaemshka na pengne mpenzi wake hamridhishi nayo inachagia sana.

Samantha Shyroh Mary:
 kama vile huwezi jitengeza nywele we mwenyewe, the same case applies on pedicure, you can’t be able to accomplish everything that is needed!
Rukia Ali: hahaha makubwa haya mayb hawakuwi satisfied na waume zao.

Sele Rnb: Kwaiyo samantha kama huwezi kujtengeneza mwnywe ndo uachie mlango wako wazi?


Carymie Paulyne Lyniedo: shida iko wapi???
Alfer Inzaghi: Nafanya hiyo kazi na nina customer ambaye unilipa hadi nikilala naye ni kazi nzuri sana.

Nassir Ahmed Allshandy: Wanawatengeneza kucha wanawatekenya wanawagonga. Kuna stile fulan yakutengeneza kucha ukimgusa tu mwanamke lazima umchape.

David Njogu Many:
 women wakuwanga small minded,very petty, vitu ndogo ndogo zinafanya watoe c***pi.

Fatya Fetty: mm nadhani kuto jiheshimu na kuto kujitambua thamani ya mwili wako.
Read more >>
Pages (38)1234 »
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger